14/05/2014
POLISI WAMGUNDUA KINARA WA MTANDAO WA WIZI KATIKA MABENKI JIJINI D’SALAAM (PICHA YAKE YATOLEWA HADHARANI) ANATAFUTWA NA JESHI LA POLISI
Jeshi la Polisi Kanda Maalum D’Salaam limefanikiwa kumbaini mtuhumiwa
mhimu ambaye ni kinara wa mtandao wa wizi katika mabenki ambaye
anajulikana kwa jina la RONALD S/O MOLLEL, umri miaka 37, mfanyabishara na
mkazi wa Kimara Bonyokwa Jijini D’salaam.
Mtuhumiwa huyu amekimbilia mafichoni mara baada ya tukio la ujambazi
katika Tawi la Benki ya Barclays Kinondoni lililotokea tarehe 15/4/2014
ambapo majambazi walifanikiwa kupora kiasi kikubwa cha fedha
T.Shs.390,220,000/= , USD 55,000/= na EURO 2150/=.
Aidha sasa imefahamika kwamba mtuhumiwa huyu ni mume wa mtuhumiwa wa kwanza katika tukio la Barclays Benki aitwaye ALUNE D/O KASILILIKA @ ALUNE D/O MOLLEL , miaka 28, Mkazi wa Kimara Bonyokwa ambaye ni Meneja wa Benki Tawi la Barclays Kinondoni.
RONALD S/O MOLLEL, mtuhumiwa wa ujambazi katika mabenki mbalimbali jijini Dar es sSlaam, anayetafutwa na Polisi.
**
Mtuhumiwa Mollel anatafutwa kwa kila hali kwa vile yeye ndiye alikuwa kinara wa kupanga tukio hilo la Barclays na mara baada ya tukio ametoroka na kiasi kikubwa cha fedha hizo zilizoibiwa.

Zipo taarifa za kuaminika kuwa mtuhumiwa huyu amekuwa akipanga na
kushiriki kikamilifu katika matukio mbali mbali ya uhalifu mkubwa ikiwa
ni pamoja na kuongoza vikundi vya majambazi vilivyowahi kupora katika
mabenki mbalimbali katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
Mtuhumiwa
huyo ni hatari kwani ana mtandao na watumishi muhimu katika matawi mbalimbali ya mabenki kwa lengo la kufanikisha uhalifu katika mabenki
hayo.
Jeshi la Polisi limelazimika kutoa picha yake hadharani kwa kutumia
dhana ya ulinzi shirikishi ili mtuhumiwa huyu akionekana akamatwe na
taarifa zitolewe katika kituo chochote cha Polisi ikiwa ni lengo la
polisi kupambana na uhalifu katika dhamira yakuzuia uhalifu, kulinda
maisha na mali za wananchi.
Zawadi nono ya fedha taslim itatolewa kwa
siri kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa
kwa mtuhumiwa huyu.
Pamoja na maelezo hayo mtuhumiwa mwenyewe sasa
anapewa fulsa ya kujisalimisha katika kituo chochote cha polisi kabla ya
kukamatwa kwa njia nyingine
Post a Comment