0

 

Halima Yahaya ‘Davina’.

BAADA ya staa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma kutoa shukurani kwa wasanii wenzake zilizotafsiriwa kama anajitabiria kifo chake, msanii mwenzake, Halima Yahaya ‘Davina’ ameibuka na kumtaka asikate tamaa.

Staa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma.
 Alisema alishtuka baada ya kuona maelezo gazetini (Ijumaa Wikienda) ambayo Wastara alimpongeza kama rafiki mwenye mchango na hakujua kama anathamini na kukumbuka vitu watu walivyomfanyia ila kikubwa amemtaka asikate tamaa kwa yote yaliyomtokea.
“Asikate tama, mitihani tumeumbiwa wanadamu, tunapaswa kuishinda,” alisema Davina.

Post a Comment

 
Top