Miss Tanzania 2013, Hapiness Watimanywa, ameibuka na kusema kuwa
kunyakuwa taji la urembo wa Miss Tanzania sio tiketi ya kuwa na skendo
mbalimbali au kufanya mambo ambayo ni kinyume na maadili.
Miss Tanzania 2013, Hapiness Watimanywa.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Happy alisema kuwa anaamini siyo
kwamba mtu anapopata taji la urembo ndiyo linampa kichwa cha kuwa
mcharuko, bali inategemea na uelewa wa mtu na mtu.
“Mimi
sitaki kuamini kabisa kuwa unapokuwa mrembo ndipo tabia chafu zinaibuka
bali ni malezi ambayo yanatofautiana miongoni mwetu,” alisema.
Mrembo huyo akaongeza kuwa, kwa upande wake anaamini atamaliza mwaka
wake wa urembo akiwa ni msafi na wanaosubiria ang’are kwa skendo
watasubiri sana
Post a Comment