Mwanamitindo
ambaye ni mchumba wa Kanye West, Kim Kardashian juzi (March 11) alipata
ajali ya gari ambayo haikuwa na madhara makubwa wakati akiendesha gari
lake aina ya Mercedes G Wagon na kukwaruzana na Nissan Sentra.
Hata
hivyo, gari la Kim Kardashian halikuharibika zaidi mkwaruzo mdogo
iliupata lakini Nissan Sentra inadaiwa kuharibika vibaya sehemu ya
mbele.
Shuhuda
wa tukio hilo ameiambia TMZ kuwa Kim Kardashian alikuwa anakata kona
kuelekea kushoto wakati dereva wa gari aina ya Nissan alikuwa anaonesha
ishara ya kuelekea kulia, lakini kwa bahati mbaya badala ya kulekea
kulia alinyooka na barabara na kulifikia gari la Kim K na kusababisha
magari hayo kukwaruzana.
Imeelezwa
kuwa wawili hao waliendesha hadi Beverly Hills Hotel ambapo
walizungumza na kuyamaliza na kila mmoja akaendelea na safari yake bila
polisi kuhusika.
Post a Comment