Mtu
mmoja amefariki dunia na wengine 38 kujeruhiwa, kati yao 14 vibaya,
baada ya magari matatu waliyokuwa wakisafiria, kugongana, mawili uso kwa
uso, huku jingine likijaribu kukwepa ajali, katika eneo la Bwawani,
barabara kuu ya Morogoro-Dar es saalam, wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
ITV imefika eneo la tukio na kushuhudia magari
mawili kati ya yaliyohusika na ajali, yakiwa yameharibika vibaya, hasa
sehemu ya dereva, ambapo mkuu wa usalama barabarani Chalinze mkoani
Pwani, Inocent Sule, amesema chanzo cha ajali ni basi la abiria, mali ya
kampuni ya Linowele class, lililokuwa likitokea dar es salaam kuelekea
malinyi wilayani ulanga, , likiendeshwa na mtu aliyefahamika kwa jina
moja la musa kujaribi kulipita gari jingine lililokuwa mbele na kukutana
uso kwa uso na tenka la mafuta aina ya Iveco, ambapo dereva wa tenka,
ali hassan ngoma, mkazi wa korogwe mkoani tanga, amefariki dunia papo
hapo, huku yule wa basi hali yake ikiwa ni mbaya sana na la tatu mali ya
kampuni ya adventure aina ya nisan diesel, lililokuwa likitokea Dar es
salaam kuelekea Kigoma liliyagonga magari hayo yaliyokuwa yamepata
ajali.
Mashuhuda wa ajali hiyo, wakiwemo majeruhi
walionusurika kifo katika ajali hiyo, ambao baadhi yao wamekimbizwa
kupatiwa huduma ya kwanza katika zahanati ya magereza bwawani,
wamezungumzia kuhusiana na namna walivyobaini ajali hiyo, huku mganga wa
zahanati ya sekondari ya magereza Bwawani, Lazaro Mdeka, akikiri
kupokea majeruhi 38, na 14 hali zao ni mbaya na wamekimbiza hospitali ya
rufaa ya mkoa wa morogoro kwa matibabu.
Katika hospitaliya mkoa wa Morogoro, huduma za
kuwapokea na kuwahuduma majeruhi hao zimekutwa zikiendelea, huku wengi
wakishindwa kuzungumza kutokana na hali mbaya.
Post a Comment