Sasa hivi imekua ni kawaida mtu kutumia pesa nyingi labda kumpeleka
mpenzi wake kwenye mahotel makubwa au kumnunulia vitu vya thamani ili
kumuonyesha mapenzi, ila ukweli ni kwamba unaweza ukafanya hayo yote
ukajiingiza kwenye gharama kubwa na matumizi usiyotarajia bila
mafaniko. Mwanamke haitaji vyote hivyo mwanamke anahitaji muda, tumia
muda mwingi kuwa nae, muonyeshe unamjali, tatizo lake chukua liwe lako.
Mpe kidogo ulicho nacho na kitoke moyoni, Usilazimishe mambo utamboa,
fanya ajiamini ukiwa nae, kuwa na misimamo yako usiyumbe yumbe katika
maamuzi, Usiogope kumwambia hisia zako kwake, kwani wanawake wanapenda
mtu anayejiamini. Fanya hayo utaona matokeo yake..!!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

Post a Comment