Home
»
WASANII
» IRENE UWOYA NDANI YA NDOA TENA NA BONGE YA TAJIRI WA MADINI
 |
Irene Uwoya
Baada ya kudaiwa kutengana na aliyekuwa mumewe yaani Ndikumana Katauti
toka nchini Rwanda, Star mkubwa wa filamu Swahiliwood Irene Uwoya
anadaiwa kuwa katika mishe mishe za kufunga ndoa na jamaa mmoja
mfanyabiashara wa Madini mwenye pesa zake ambaye anaishi Sinza, Dar es
salaam. Habari zaidi zinadadavua kuwa jamaa huyo
ameoza kwenye penzi la Uwoya ambaye alifunga ndoa ya kifahari na
Ndikumana miaka michache nyuma na kuishia kuwa katika gogoro la mara kwa
mara. Jamaa ndiye anataka kumuoa Uwoya haraka iwezekanavyo huku
mashosti wa Uwoya wakimshangaa star huyo kama ataiweza ndoa hiyo baada
ya kushindwa kwa Ndiku. "Inashangaza sana kwasababu hata Uwoya mwenyewe
anaridhia hicho kitu, sasa sisi mashosti zake tunajiuliza alishindwa
nini kwa Ndiku mpaka leo hii atake kuingia kwenye ndoa mpya?" Chanzo
kililiambia gazeti la Visa
Chanzo hicho kilizidi kumwaga habari
kwa kusema "huyo kijana kadata na Uwoya kwa kweli, hasikii la bibi yake
wala la shangazi zake, kaamua na yeye ndiye kiherehere kutaka kumuoa
Uwoya, na hizo pesa zake ndizo zinazomzuzua hata Uwoya mwenyewe"
Mashosti hao wa Uwoya walimalizia kwa kusema kuwa hata hivyo Uwoya
atakuwa na wakati mgumu kwani mpaka sasa wazazi wake hawajui kuhusu
issue hiyo ya ndoa mpya kwasababu wao ni waaminifu kwa dini yao ya
kikiristu na pia bado wanamtambua Ndikumana kama mkwe wao kwasababu ndoa
za kikiristu huwa hazivunjiki. |

Filamu kali ya SIO SAWA inaingia sokoni tarehe 24 April 2014 hakikisha unanunua nakala yako halisi.
Post a Comment