CHAMA cha siasa cha Alliance for Change and Transparency ( ACT-Tanzania ) ambacho kinatajwa kuasisiwa na mwanasiasa machachari, Zitto Kabwe na vigogo wa zamani wa CHADEMA, jana kilipatiwa usajili wa kudumu na msajili wa vyama vya siasa nchini,Jaji Francis Mutungi....
Jaji
Mutungi alikabidhi cheti cha usajili wa kudumu kwa kaimu
mwenyekiti wa chama hicho, Kadawi Limbu katika hafla iliyofanyika
mjini Dodoma jana....
Kuhusishwa kwa Zitto Kabwe na ACT-Tanzania
Habari
za kuaminika kutoka ndani ya chama hicho zinaeleza kuwa Zitto
ambaye ni mbunge wa Kigoma kaskazini kupitia CHADEMA ndiye
mlezi wa chama hicho....
Pia
mjumbe wa zamani wa kamati kuu ya CHADEMA,Dr. Kitila Mkumbo
naye anaelezwa kuwa mwanachama mwanzilishi wa chama hicho....
Zitto
na Kitila wanahusishwa na chama hicho baada ya kuvuliwa
uanachama wa CHADEMA Novemba 22 mwaka jana kwa kutuhumiwa za
kula njama za kuhujumu chama hicho....
Hata hivyo Zitto alipinga uamuzi huo na kuamua kufungua kesi mahakama kuu kupinga kuvuliwa uanachama wake...
Ukweli
wa Zitto kuwa karibu na chama hicho unajionyesha zaidi
kutokana na wadhifa wa katibu wa muda wa ACT-Tanzania kushikwa
na Samson Mwigamba,ambaye alivuliwa vyeo vyake kutoka CHADEMA
pamoja na Zitto na Dr. Mkumbo kwa tuhuma zinazofanana....
Bila
kusahau kuwa wanachama wengi wa ACT-Tanzania wanaelezwa kuwa
wanatoka katika baadhi ya mikoa ambayo ilikuwa chini ya
Zitto,wakati alipokuwa mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya
magharibi...
Alipoulizwa
juu ya habari ya Zitto kuwa mlezi na Kitila kuwa mwanachama,
Mwigamba hakukiri wala kukataa juu ya jambo hilo....
"Hayo
mambo ya nani ni mwanachama wetu kwa sasa siwezi
kuyazungumzia.Jambo muhimu hapa tumepata usajili wa kudumu"
Alisema Mwigamba ambaye alijibu kwa nia ya simu kutoka Arusha
ambako alikuwa kwa shughuli binafsi na kumfanya akose shughuli
ya kukabidhiwa cheti cha usajili...
Msajili ataka siasa za ukomavu
Akizungumza
kabla ya kukabidhi cheti hicho, Jaji Mutungi aliwataka viongozi
wa chama hicho kufanya siasa zenye ukomavu kwa kuzingatia
sheria ya vyama vya siasa na kanuni zake
Jaji
Mutungi aliwataka pia viongozi hao kuwaheshimu wanachama wao
kwa kuwa vyama vingi vikishapata usajili viongozi huwasahau
wanachama wao....
"Mmepata usajili, mmeikuta nchi yetu ina amani hivyo tunaomba mfanye siasa ambazo zitahakikisha nchi inaendelea kuwa na amani," alisema Jaji Mutungi akitaka chama hicho pia kishiriki katika kutoa maoni ya kuzifanyia marekebisho sheria ya vyama vya siasa na sheria ya gharama za uchaguzi
Kwa
upande wake msaidizi wa msajili wa vyama vya siasa,Sisty
Nyahoza,aliipongeza ACT-Tanzania kwa kutimiza masharti na
hatimaye kupata usajili wa kudumu...
Alisema
chama hicho kilifanikiwa kuleta wanachama zaidi ya 200 katika
mikoa 10 ya Tanzania Bara na mikoa miwili kutoka Tanzania
Visiwani...
"Epukeni
kujihusisha katika vurugu, sheria inakataza vyama vya siasa
kutumia nguvu katika shughuli za siasa,hali hiyo inafifisha
demokrasia na kuwatia hofu wanachama" alisema
Akizungumza
mara baada ya kupokea cheti cha usajili wa kudumu,Limbu
alisema chama hicho kimepanga kufanya demokrasia ya kweli
nchini...
"Chama
chetu hakitakuwa chama cha vurugu,kitakuwa ni chama cha
heshima,hakitakuwa na mmiliki,kitakuwa ni chama cha wanachama,
hatutegemei migogoro na tutafanya siasa za kistaarabu" Alisema Limbu
Akizungumzia chama hicho kuwa na watu maarufu nyuma yake,Limbu alisema hayo ni masuala ya kusikia.
"Sisi
ni wanasiasa wazoefu,tunajiamini,hatuna sababu ya kufanya kazi
kwa kuwa kuna watu nyuma yetu wanategemewa kuwa viongozi"
"Tunaamini wapo
watu na viongozi wa vyama vingine wanakerwa na demokrasia
ndani ya vyama vyao,vipo vyama ambavyo ni makampuni ya watu,
ukionekana kugusa maslahi ya mtu unafukuzwa, tunawakaribisha waje
tujenge demokraia.
"Tunaamini
watu wa namna hiyo ni moja kati ya chachu ya watakaokuja
kujenga chama chetu,tunamhitaji mtu yeyote mwenye uwezo na
nguvu, atakayejenga demokrasia ya kweli" alisema
ACT yaanza na wanachama 4,200
Mwigamba alisema chama hicho chenye mlengo wa kati-kushoto kina wanachama 4,200 kutoka mikoa 13 ya Tanzania Bara na Zanzibar....
"Chama chetu kinaamini katika ujamaa na demokrasia jamii,yaani tunataka kurudisha u-Nyerere" alisema Mwigamba ambaye alitaja kauli mbiu ya chama hicho ni 'Tanzania Kwanza,Uwazi na Mabadilko',


Post a Comment