0


Watu wa karibu wa Mtuhumiwa huyu walijitokeza Mahakamani ili kuangalia kama ndugu yao aitwae Simon Ngozi (21) ataweza kupata dhamana kwenye kesi inayomkabili ya kubaka mtoto wa miaka tisa.

 
Jamaa alikua amepelekwa Mahakamani Makadara Nairobi   nchini  Kenya  lakini ghafla akamshangaza kila mtu baada ya kutaka kumbaka Mwanamke aliyekua karibu yake baada ya kuanza kumshikashika.

Mshukiwa huyu alikuwa kortini kujibu tuhuma za kumbaka mtoto wa miaka tisa April 2014 ambapo wakati anataka kumbaka Mwanamke huyu Mahakamani tena kwenye eneo la wazi, alimpiga mtama kwanza Mwanamke huyo lakini kwenye purukushani zake hakufanikiwa manake Polisi walimuwahi.
 
Shughuli za Mahakama zilisimama kwa muda baada ya tukio hilo kutokea ambapo baada ya hapo Mwanamke aliyetaka kubakwa alisema, "Nilikua nimeketi karibu naye na mara ya kwanza alilishika begi langu nikalisogeza mbali nikidhani ni mwizi lakini bila aibu akanishikashika tumboni kabla ya kunisukuma nikaanguka sakafuni"
 
Baada ya hapo dada wa mtuhumiwa alimuomba mwanamke huyo kumsamehe ndugu yake akisema yuko katika hali hiyo baada ya mchumba wake kumtoroka kwa sababu ya kesi ya ubakaji.

Post a Comment

 
Top