Tukio hilo limetokea wakati wakikagua magari jirani na transimita ya kituo cha TBC Songea katika eneo la mshangano mkoani Ruvuma.
Hata hivyo polisi kwa kushirikiana jeshi la wananchi wamefanikiwa kutegiua bomu hilo.
Kutokana na kishindo kikubwa wakati wa kuliharibu bomu hilo mwanafunzi wa shule ya jirani na lilikotegwa bomu hilo Malizia Konja alizimia na anaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya mkoa wa Ruvuma.
Tukio hilo linatokea zikiwa zimepita siku chache baada ya askari polisi wawili kujeruhiwa vibaya kwa bomu la kienyeji ambapo kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma ACP Mihayo msikhela anasema polisi kwa kushirikiana na jeshi la wananchi wamefanikiwa kuliharibu bomu hilo…
Muuguzi wa hospitali ya mkoa Agnes Charles amethibitisha kumpokea mwanafunzi Malizia Konja huku mwanafunzi huyo akieleza ilivyokuwa baada ya kusikia kishindo cha bomu hilo.

Post a Comment