Mahsein Awadh ‘Dk Cheni’ akiwa hoi hospitalini.
Akizungumza wikiendi iliyopita Dk Cheni alisema
kuwa alikuwa mshehereshaji (MC) kwenye harusi moja iliyofanyika maeneo
ya Sinza jijini Dar ndipo akala chakula hicho ambapo muda mfupi baadaye
alianza kujisikia vibaya ‘kichina’.Staa huyo alisema kuwa baada ya hatua chache kutoka ukumbini, tumbo lilianza kumuuma kisha akaishiwa nguvu ndipo akaweka gari pembeni na kupiga simu kwa ndugu kuomba msaada.
Dk Cheni aliendelea kueleza kuwa baada ya kupata msaada moja kwa moja alipelekwa kwenye Hospitali ya Burhani jijini Dar.
‘Dk Cheni’,
Alisema kuwa baadaye alihamishiwa kwenye Hospitali ya TMJ ambapo
madaktari walipompima waligundua alikuwa amekula chakula chenye sumu
ndipo wakampatia matibabu na kulazwa.Alisema siku ya pili yake aliruhusiwa huku akisema kitendo hicho kimemsikitisha mno.
Siyo mara ya kwanza kwa Dk Cheni kulishwa chakula chenye sumu kwani safari hii ni mara ya pili ambapo mwaka jana alilazwa tena kwa ishu kama hiyo, jambo ambalo haelewi kwa nini inakuwa hivyo
Post a Comment