0
Ukijaliwa kuwa Msichana mzuri na mrembo,usidhani utatetemesha kila Mwanaume, kuna wanaume na akili zao kichwani,urembo wako hauwasumbui,kama bichwa lako ni kanyaboya,uzuri wako hausaidii kitu,na utashangaa no one is paying attention,watu utakaowapata ni
walewale kanyaboya wenzako, na hawana futuretabaki unaliwa bure kila siku unatoa macho.

Ukipata mwanaume anakupenda unaanza drama zako na kupiga watu danadana,madai yako hujali na unadhani hata akiondoka utapata

mwingine kisa wewe ni mzuri,la hasha! Mwanaume akijitoa mhanga
kukupenda kwa uzuri wako mheshimu,maana viumbe wa kike
wakiwa wazuri ni shida na matatizo hakuna mtu anataka,sasa

ukimwongezea na drama pamoja na yeye kujigeuza mpalestina kwako
utajikuta umeolewa na kioo cha chumbani kwako,maana hicho ndo
kinakudanganya sana kwamba we ni mrembo, Watch out, drama zina
mwisho,leo unacheza na mioyo ya watu unajiona we kifaa,usidhani
wanaume hawaumii, tunaumia sema hatusemi tu,machozi yetu kama ya samaki, tunalia ndani kwa ndani.

Post a Comment

 
Top