0
Utafiti mpya uliotolewa nchini Marekani, umebainisha kuwa watu wanaopenda kulala bila nguo wanapata faida nyingi ikiwamo ya kuwa na uwezekano mdogo wa kupata ugonjwa wa kisukari.
Ripoti hiyo ya utafiti iliyotolewa na Taasisi ya Kitaifa ya Usingizi (NSF), inaeleza umuhimu wa watu kulala bila nguo kuwa ni kuimarisha uhusiano kwenye ndoa na kupunguza kalori nyingi.
Wataalamu wa usingizi wanasema kwamba ni vizuri mtu akawa katika hali ya utulivu wakati wa usiku kwa kuwa joto la mwili linahitaji kuteremka hadi nyuzi 50 za kipimo cha Fahrenheart ili mtu aweze kulala.

Wakati ubongo ukiendeshwa kwa ‘saa’ iliyo ndani ya mwili, hutuma ujumbe kuutaka moyo ufunguke au kufunga
“Joto la mwili huwa juu saa 5 usiku na kuwa chini saa 10 asubihi,” anasema Mkurugeni wa Edinburg Sleep Centre, ambaye pia ni mwandishi wa Kitabu cha Sound Asleep, Dk Chris Idzikowski.
“Kama kitu chochote kitazuia joto lisishuke, ubongo utahakikisha unajua kinachoendelea, hii inamaanisha, utahangaika kupata usingizi au utakuwa na usingizi wa mang’amunga’amu,” anasema mtaalamu huyo.
Ripoti hiyo inasema kuwa mtu anapolala bila nguo inakuwa rahisi kwa mwili kupoa na kuwezesha upatikanaji wa kiwango sahihi kinachohitajiwa na ubongo kufanya kazi.
Profesa Russell Foster, mtaalamu wa circadian neuroscience katika Chuo Kikuu cha Oxford, anathibitisha kuwa kulala bila nguo kunaboresha usingizi.
“Kama ulikuwa unavaa nguo nyingi za kulalalia, itakuwa vigumu kwako kupunguza joto. Kwa hiyo, punguza nguo unavyoweza,” anasema.
Anasema kuwa ikiwa usingizi umekatishwa kwa sababu ya joto kali, haimaanishi kwamba utapata usingizi mdogo wakati wote, bali unaweza kupata usingizi wa kushtuka shtuka.

Usingizi mzuri ndiyo unaofaa kwa ajili ya kuimarisha mfumo wa kumbukumbu na uzalishaji wa homoni, kitendo ambacho ni muhimu kwa ukuaji wa seli na kuzifanyia marekebisho.
Kwa nini mwili unapoa wakati umelala?
Utafiti unasema kuwa siyo vizuri kuoga maji ya moto jioni wakati wa kwenda kulala, badala yake mtu anapaswa kupasha moto kigodo mikono na miguu yake. Hiyo ni kwa sababu ili joto la mwili lishuke hadi kufikia kiwango cha chini kinachochochea usingizi, mwili unatakiwa utoe jasho.
“Jambo hili linafanyika kwa kutuma damu kwenye mishipa karibu na ngozi- hasa kwenye mikono na miguu, ambako joto linapotea kwa njia ya ngozi,” inasema ripoti hiyo.
Hata hivyo, kama Profesa Foster alivyoeleza, kama mikono na miguu yako ni baridi, mishipa ya damu karibu na ngozi itapunguza kasi ya damu kutembea katika harakati za kutafuta joto na kuzuia lisipotee.
“Hii ina maanisha kuwa joto lako la kawaida haliwezi kushuka kirahisi,” inasema ripoti.
Taarifa hiyo inasema kwamba ndiyo maana watu wenye ugonjwa wa kuwa na mikono na miguu ya baridi sana (ugonjwa huo unawaathiri zaidi ya watu milioni 10 Uingereza, asilimia 10 wakiwa ni wanawake), ambao ndiyo wenye hatari zaidi ya kupata ugonjwa wa kukosa usingizi, ‘insomnia’.
Hali hiyo husababisha mishipa ya damu kusinyaa, kupunguza kasi ya damu kutembea, kwa hiyo ingawa watu wanaosikia mikono yao ni ya baridi sana, joto lao huwa juu sana.
Ripoti hiyo inaendelea kufafanua kuwa wazee wana kawaida ya kujisikia baridi usiku, labla kwa sababu matatizo ya mzunguko wa damu kwao ni kawaida.
“Wanawake ndiyo wenye hatari zaidi ya kupatwa na matatizo ya baridi mikononi na miguuni, hasa wakati fulani wanapokuwa kwenye hedhi.
Utafiti mwingine uliofanywa mwaka 2008 na Taasisi ya Netherland inayojishughulisha na Sayansi ya Neva, pia unaeleza uhusiano wa joto la mwili na kulala.
Kuna baadhi ya watu walijitolea kuvaa nguo zinazozuia mabadiliko ya joto la mwili, ili kuwaruhusu watafiti kuchunguza joto kwenye ngozi bila kuathiri kiwango cha kawaida cha joto mwilini.
Timu ya watafiti hao waligundua kuwa wakati joto kwenye ngozi linapopanda kwa nyuzi 0.4, watu waliokuwa wanafanyiwa utafiti walikuwa na uwezekano mdogo wa kuamka wakati wa usiku. Lilipojitokeza kundi la wazee kufanya majaribio kama hayo, matokeo yalishangaza. Joto lilipofikia nyuzi 0.4, lilikaribia kuwa mara mbili ya hali ya kawaida ya kulala, pia lilipunguza uwezekano wa kuamka mapema kwa asilimia 50 hadi nne.

“Joto kwenye ngozi lilipoongezeka lilisababisha mirija ya damu kupanuka, hivyo joto kupotea kwa urahisi zaidi. Waliongeza uwezo wa kulala kwa kuongeza joto na kuruhusu kasi yake kutembea kutoka katikati ya mwili,” anasema Profesa Foster.
Chanzo: Mwananchi

Post a Comment

 
Top