Rais Barack Obama wa Marekani ambaye hupenda kujichanganya mara kwa mara na kuonesha jinsi anavyotaka kuwafikia watu aina zote, hivi karibuni alifanya mahojiano na Zach Galfianakis katika kipindi cha ‘Between Two Ferns’ kinachowekwa kwenye mtandao.
Kipindi hicho ambacho huwa na maswali mengi ya kejeli na ya kukwaza wakati mwingine, huwekwa kwenye tovuti ya Funny or Die.
Tovuti
hiyo imeeleza mwishoni mwa wiki kuwa kipindi alichofanya Zach
Galfianakis na Barack Obama na kuwekwa kwenye akaunti yao ya YouTube
kimeangaliwa zaidi ya mara milioni 15 na hivyo kinaonesha dalili ya kuwa
kitavunja rekodi ya mahojiano na Justin Bieber ambaye kipindi chake
kilifikisha viewers milioni 17.8.
Baada
ya kufanya mahojiano na kipindi hicho na kutupiwa maswali kadhaa ya
kejeli, Ijumaa ya wiki iliyopita Obama alimwambia Ryan Seacrest katika
mahojiano kuwa kwa kufanya vile anaamni ameweza kuwafikia vijana wengi
na ujumbe wa sera yake ambapo hata binti yake Malia alikuwa amevutiwa
baada ya kusikia kuwa amerekodi kipindi na Galfianakis.
Obama alipata nafasi ya kuzungumza kuhusu sera yake ingawa asilimia 97 ya mahojiano ilijaa kejeli na maswali ya ucheshi.
Post a Comment