Tishio
la kigaidi lina kodolea macho taifa la Kenya baada ya kundi la kigaidi
lililo na makao yake makuu nchini Somalia kuachia video nyingine kwenye
mtandao wa Al-Kataib wakitishia kutekeleza mashambulizi nchini Kenya
wakati wowote.
kwenye
kanda hiyo msemaji wa alshabaab aliye jifunika uso anasema kwamba
hawaoni lolote litakalo wa zuia kuingia Kenya hasa baada ya kufanikiwa
kutekeleza mauaji katika jengo la west Gate. mwaka
uliopita>>’tumekuwa tukisema tutafika Kenya lakini hivi tayari
tushafika si eti westgate ndio tosha bado kuna mamia na mamia ya watu
wanaongojewa mahala kama hiyo insha Allah’alisema msemaji huyo.
Huku
wakiimbia tutawalipua hadi tuwamalize wanamgambo hao wamesema kwamba
wameamua kuungana na wasomali kutetea dini ya Allah,Wadadisi wa maswala
ya kiusalama wanahoji kwamba huenda hawa ni baadhi ya vijana kutoka kwa
mataifa ya Afrika mashariki walipewa mafunzo ya itikadi kali na baadaye
kupelekwa somalia kujiunga na Alshabaab kutokana na wanavyozungumza
lugha ya Kiswahili kwa ufasaha kwenye video hiyo.
Ispekta
mkuu wa polisi nchini Kenya bwana David kimaiyo amesema uchunguzi
umeanzishwa kubaini chanzo cha video hiyo na taarifa kamili kutolewa
punde tu watakapo pata habari zaidi kuhusiana na video hiyo.
CREDIT: XDEEJAYZ TANZANIA
Post a Comment