MSANII
wa filamu Bongo, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ hivi karibuni alijikuta
akichezea kichapo kutoka kwa mpenzi wake anayejulikana kwa jina la Amani
baada ya kutaka kwenda klabu usiku bila kumtaarifu.
Msanii wa filamu Bongo, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ akipozi.Kwa mujibu wa majirani, tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki
iliyopita ambapo walimsikia msanii huyo akipiga mayowe na walipotoka
walimuona akipigwa.“Kwa kweli alipigwa sana na sasa amevimba uso,” alidai mmoja wa majirani aliyeomba hifadhi ya jina lake.Paparazi wetu alimtafuta Aunty Lulu lakini hawakuweza kuonana naye
kwani aligoma akidai kwa hali aliyonayo hawezi kuonana na waandishi ila
akasema:“Ni kweli Amani kanipiga, kaniumiza ila siwezi kuliongelea sana suala hilo, haya ni mambo yetu binafsi.”
Post a Comment