0


Maskini! Mzee aliyefahamika kwa majina ya London Haonga (61) mkazi wa Kijiji cha Mapogolo, Kata ya Mbebe wilayani Ileje mkoani
hapa hana tena nyeti zake kufuatia tukio la kukatwa sehemu hizo lililokuwa kama sinema, Amani lina ripoti kamili. Kwa mujibu wa shuhuda wetu kijijini hapo, tukio hilo la kusikitisha lilitokea mishale ya saa mbili usiku wa Aprili 19, mwaka huu mzee huyo alifanyiwa unyama huo na watu watatu wasiofahamika kisha kutokomea nazo kusikojulikana.
Mzee aliyefahamika kwa majina ya London Haonga akikimbizwa hospital baada ya kukatwa nyeti.
HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA
Shuhuda wetu alisema mmoja wa watuhumiwa alifika nyumbani kwa mzee huyo, akabisha hodi akidai kupotea njia hivyo akawa anaomba msaada wa kuelekezwa.Bila kujua atapoteza nyeti, mzee London alitoka nje ya nyumba yake akiwa anamwelekeza njia mtu huyo mita chache kutoka nyumbani kwake.
Gari la wagonjwa lililombeba mzee ondon Haonga.
Ghafla alipigwa na butwaa aliposikia kishindo cha watu wakimrukia na kumziba kwa kitambaa cheusi usoni kisha kumwangusha na kumfunga kamba.
Baada ya kufanikiwa kumtuliza na kumbana kisawasawa ndipo wakachukua kisu na kumkata sehemu zake za siri ambazo waliondokanazo.
Kwa mujibu wa shuhuda huyo, Mtendaji wa Kijiji cha Mapogolo, Cosmas Haonga alipofika alimkuta mzee London akiwa amepoteza fahamu na alipozinduka alipiga mayowe kuomba msaada.Majirani nao walifika na kutoa msaada wa kumkimbiza Hospitali ya Wilaya ya Ileje huku wakiwasaka watuhumiwa wa unyama huo.
Kwa mujibu wa mtendaji huyo wa kijiji, watuhumiwa hao wanadaiwa wanatokea Mpemba wilayani Momba ambao walitambuliwa na mwathirika wa tukio hilo ambapo baada ya kupewa PF-3, mzee London alikimbizwa Hospitali ya Rufaa Mbeya.
Alipofikishwa hospitalini hapo majira ya saa 11:00 jioni alikuwa akilalamikia maumivu makali.
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa chanzo cha awali imedaiwa sababu ya kutendewa ukatili huo umetokana na mmoja wa ndugu aliyedai kuwa mzee huyo anatuhumiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mke wa mdogo wake hivyo watu hao walitumwa kwa nia ya kulipiza kisasi.
Aidha, ilidaiwa kuwa baadhi ya viungo vimekamatwa na wengine kudai kuwa tukio hilo kuhusishwa na imani za kishirikina kwani watuhumiwa walidaiwa kumbilia nchi jirani lakini kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, SACP Ahmed Msangi, alisema jeshi la polisi linawasaka kwa udi na uvumba.

Post a Comment

 
Top