Home
»
WASANII
» FLORA AFUNIKA KWA MAUNO SIKU YA BUNYEROBUNYERO
Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Flora Mvungi.
MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Flora Mvungi amenaswa akiwafunika vibaya mastaa wenzake kwa kunengua.
Mpambano huo usio rasmi ulichukuwa nafasi wiki iliyopita katika Ukumbi wa New Maisha, Masaki jijini Dar ambapo kulikuwa na shoo maarufu kwa jina la Bunyerobunyero.
Flora alipoulizwa na mwanahabari wetu juu ya ufundi huo wa kucheza Kibao Kata kilichokuwa kikipigwa na kuwazidi mastaa kama Kajala Masanja, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ na Halima Haroun ‘Kimwana’, hakuwa tayari kujibu zaidi ya kuendelea kukatika.
Post a Comment