Home
»
MICHEZO
» HILI NI PIGO KWA TIMU YA CHELSEA, RAMIRES AFUNGIWA MECHI NNE ZA LIGI
RAMIRES AKIMCHEZEA NDIVYO SIVYO LARSSON
Klabu ya Chelsea imepata pigo katika mbio zake za kusaka ubingwa wa EPL baada ya
kiungo wake mahiri raia wa Brazil Ramires kufungiwa michezo minne ya ligi na
chama cha soka England FA.
FA imefikia hatua hiyo baada ya uchunguzi uliofanywa
kupitia picha za Television kumuonyesha kiungo huyo akimfanyia madhambi mchezaji
wa klabu ya Sunderland Sebastian Larsson katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa
katika uwanja wa Stamford Blidge na Chelsea kulala kwa mabao 2-1.
Katika mchezo
huo uliofanyika jumamosi ya tarehe 19 mwamuzi wa kati Mike Dean hakuweza kuliona
tukio hilo kutokana na umbali uliokuwepo kati yake na tukio lenyewe.
Ramires
amekubaliana na adhabu hiyo hivyo atakosa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Liverpool
jumapili hii kisha mchezo dhidi ya Norwich City utakaofuatiwa na mchezo wa
kufunga msimu wa ligi dhidi ya Cardiff City huku mchezo wa nne na wa mwisho
katika adhabu hiyo utakuwa mwezi August katika msimu mpya wa 2014-2015.
Ikumbukwe
adhabu ya kumfanyia madhambi Larsson ni michezo mitatu nje lakini FA imeongeza
mmoja na kufikia minne kutokana na Ramires kutoka katika kifungo kingine
kufuatia madhambi aliyofanya katika mchezo dhidi ya Aston Villa mwezi uliopita.
Post a Comment