NAKUKUBALI! Mkongwe kwenye soko la filamu za Kibongo, Fatuma
Makongoro ‘Bi Mwenda’ amefunguka kuwa anamzimika kinomanoma mkali wa Hip
Hop Bongo, Joseph Haule ‘Prof Jay’ kutokana na tungo zake mahiri.
Bi Mwenda aliitoa kauli hiyo Jumatano iliyopita katika hafla ya
Uzinduzi wa Global TV Online iliyofanyika katika Ofisi za Global
Publishers, Bamaga-Mwenge ambapo wasanii mbalimbali wa filamu na muziki
akiwemo Prof Jay, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’, Mahsein Awadh ‘Dk Cheni’,
Issa Musa ‘Cloud 112’ na wengine kibao walihudhuria.
Fatuma
Makongoro ‘Bi Mwenda’, Profesa J na baadhi ya wasanii wa Bongo Muvi
wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa Global TV Online
katika ofisi za Global Publishers.
“Oooh! Jamani ndiyo mara ya kwanza namuona Prof. Jay kwa macho yangu,
kiukweli nakubali sana kazi zake, ni mtunzi mzuri, mwimbaji na hata
nyimbo zake huwa zina ujumbe sana,’’ alisema Bi Mwenda.
Post a Comment