0


Habari wapendwa,kuna kitu kinanikera mpaka nimeamua kuongea na inabidi tumuogope Mungu,kuna jamaa mmoja alioa akafukuza mke wake,badae akamrudia mke wake Mungu akawajalia mtoto mmoja,wakati huyo mke ana mimba jamaa akachepuka bahati mbaya mchepuko ukapata ujauzito,jamaa akachanganyikiwa kwa sababu aliuambia mchepuko hana mke yani walishaachana,sasa jamaa akakimbilia nigeria kwa TB Joshua ili aambiwe nani mke kutoka kwa Mungu wakati mke wa kwanza alifunga nae ndoa,baada ya jamaa kurudi akatulia ndani ya miezi 6 huku akimuomba Mungu amuonyeshe,wiki 2 zilizopita kasema Mungu kamuonyesha mchepuko ndio mke wake,ila nigeria hakuambiwa kitu,sasa kwa mke halali hataki kupasikia wala habari za mtoto.

Post a Comment

 
Top