Wazanzibari, kwa upande wao wanaendelea kusema kwamba kwa kipindi
chote hicho wameshindwa kufanya jambo lolote kwa maendeleo yao kutokana
na kivuli cha muungano na kwamba kila wanalotaka kulifanya lazima
Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania itahoji.
Yapo mengi ambayo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imekuwa ikitaka kufanya baadhi ya mambo bila kupitia kwenye muungano na mojawapo ni uamuzi wake wa kutaka kujiunga na Shirikisho la Nchi za Kiislamu Duniani (Organisation of Islamic Conference – OIC) mwaka 1992.
Hapo ndipo mzozo wa mambo ya muungano ulipopamba moto. Lengo kubwa la SMZ kwa wakati ule, chini ya Rais Dk. Salmin Amour Juma, lilikuwa kuifanya Zanzibar kuwa nchi au taifa la Kiislamu, wakati inafahamu fika kwamba suala hilo lilipaswa kujadiliwa kabla ya kuchukua maamuzi mazito kama waliyofanya.
Uamuzi huo ukazua mjadala mrefu sana ndani ya Chama Cha Mapinduzi (wakati huo serikali ilikuwa bado ya chama kimoja) na hata bungeni, ambako wabunge na wana-CCM wa Bara waliona wamesalitiwa na kiongozi huyo wa Zanzibar ambaye pia ndiye alikuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM upande wa Zanzibar na pia kikatiba alikuwa ndiye Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Muungano wa Tanzania.
Lakini Zanzibar haikujiondoa OIC kama tulivyoelezwa na viongozi wetu, bali kilichotokea ni kwamba, OIC ilichunguza na kukuta kwamba Zanzibar siyo taifa linalojitegemea, yaani Sovereignty State na kwa mujibu wa masharti yao, haikustahili kuwa mwanachama, hivyo wakaiondoa.
Kujiunga kwa Zanzibar katika OIC kuliwazindua wabunge wa Tanzania Bara, ambao waliona kwamba kuwepo kwa serikali mbili ndani ya muungano kulikuwa ni kama kuwapa kiburi Wazanzibari, kiasi cha kufanya lolote wanalotaka bila kusubiri baraka za upande mwingine.
Ndipo katika kikao cha Bunge la Bajeti cha mwaka 1993, aliyekuwa Mbunge wa Chunya, Mheshimiwa Njelu Kasaka akawasilisha hoja binafsi bungeni na kudai Serikali ya Tanganyika ndani ya muungano ili kutoa uwiano sawa.
Kwa bahati nzuri, hoja hiyo ilipata baraka za Waziri Mkuu (wa wakati huo), John Samuel Malecela ‘Cigwiyemisi’ na kupitishwa na Spika wa Bunge ( wa wakati huo), marehemu Chifu Adam Sapi Mkwawa ili ijadiliwe. Ni katika mjadala huo nipo hoja ya kutakiwa uwepo wa serikali tatu tatu ikaibuka.

Post a Comment