MATESO! Mama wa kambo ametiwa mbaroni akidaiwa kumfanyia ukatili mtoto Sada Athuman (10), mkazi wa Yombo-Kilakala jijini Dar, Risasi Jumamosi lina kisa na mkasa.
Awali, gazeti hili lilipokea ujumbe mfupi (SMS) kutoka kwa chanzo
chake kuwa watu wa Ustawi wa Jamii wakishirikiana na polisi walitinga
nyumbani kwa mama huyo na kumfikisha kituo cha polisi baada ya kufanya
uchunguzi wa kina na kubaini ukatili aliokuwa akimtendea mtoto huyo.
Huku akionesha majeraha sehemu mbalimbali za mwili, Sada alidai kuwa makovu aliyonayo yalitokana na fimbo anazotandikwa na mama huyo.
Kwa upande wake baba wa mtoto Athumani Francis (35) alisema yeye alikuwa hafahamu chochote kuhusiana na malezi hayo yasiyo sahihi kwa mtoto wake aliyekuwa akichoteshwa maji hadi ndoo kumi na tano kwa wakati mmoja, jambo lililowakwaza majirani.
Mtoto Sada Athuman (10) aliyefanyiwa ukatili na mama wa kambo.
Ilielezwa kwamba baada ya kufikishwa katika Kituo cha Polisi cha
Chang’ombe, Dar, mlezi huyo alifunguliwa jalada la kesi namba
CHA/RB/2245/2014- UKATILI DHIDI YA MTOTO ambapo anasubiri kufikishwa
kwenye mkono wa sheria.
Sehemu ya mguu alipoumizwa mtoto Sada.
Katika maelezo yake, mtoto huyo alidai kuwa amekuwa akipata vipigo
vya nguvu kutoka kwa mlezi wake huyo ambaye alianza kumlea tangu akiwa
na umri wa mwaka mmoja.Huku akionesha majeraha sehemu mbalimbali za mwili, Sada alidai kuwa makovu aliyonayo yalitokana na fimbo anazotandikwa na mama huyo.
Kwa upande wake baba wa mtoto Athumani Francis (35) alisema yeye alikuwa hafahamu chochote kuhusiana na malezi hayo yasiyo sahihi kwa mtoto wake aliyekuwa akichoteshwa maji hadi ndoo kumi na tano kwa wakati mmoja, jambo lililowakwaza majirani.
Sehemu ya mkono alipoumizwa mtoto Sada na mama yake wa kambo..
Kwa upande wake Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, SACP Englibert
Kiondo alisema suala la ukatili kwa watoto linazidi kushamiri kwa sasa
hivyo wananchi wajitahidi kuonesha ushirikiano kwa kutoa taarifa katika
vyombo husika wanapoona matukio hayo.
Post a Comment