Msanii maarufu nchini Tanzania Kutoka kundi la Orijino Komedi al
maarufu kama Mpoki a k a Muarabu wa Dubai anatarajiwa kuondoka nchini
mapema mwanzo wa wiki hii kwenda nchini Ujerumani kuhudhuria Mkutano
mkuu wa Umoja wa Watanzania Ujerumani (U T U), utakaoambatana na
Kongamano la kibiashara pamoja na Sherehe za Muungano wa Tanzania ,
zitakazoanza siku ya ijumaa tarehe 25.04.14 na kumalizika siku ya
Jumamosi Tarehe 26.04.14.
Mpoki
amesema kuwa umuhimu mkubwa wa safari yake ni kuwakilisha wasanii wa
Tanzania katika Tamasha hili kubwa la aina yake, na kufafanua kuwa
wakati umefika kwa wasanii wa Tanzania kushirikiana kikamilifu na
Watanzania wanaoishi nje ya nchi ili kuweza kupata fursa mbali mbali
zilizopo huko.
Amesema amevutiwa sana na Umoja Wa Watanzania Ujerumani (U T U) kwa
shughuli zake mbali mbali ambazo umekwishazifanya nchini humo na
ameamua kutoa mchango wake wa hali na mali kuhakikisha (U T U)
inafanya vizuri zaidi na kwamba yeye binafsi amekuwa ni mfuatiliaji wa
karibu sana wa shughuli za umoja huo.
Mwenyekiti wa Umoja Wa Watanzania Ujerumani Bw. Mfundo Peter Mfundo
alithibitisha safari ya msanii huyo Maarufu nchini Tanzania, na kusema U
T U Ilipendelea sana wasanii zaidi kuhudhuria sherehe hizi lakini kwa
bahati mbaya haikuwezekana kutokana na mambo yalio nje ya uwezo wao
ingawa UTU ni chombo kinachokubali sana na kuzifagilia kazi za wasanii
wa Tanzania.
U T U inamtakia Bw Mpoki Safari njema.

Post a Comment