Nikiwa kikaoni nikasikia mtetemo kwenye sim yangu ikiashiria ujumbe mfupi umeingia,sikua na haraka ya kuusoma,nikijua baada ya kikao ntausoma,ndio ntakua na muda mzuri wa kusoma ujumbe huo,hata hivyo mimi ndie nilikua katibu wa kikao,nikakipa kikao uzito zaidi.

Nikajua mamaa kaishiwa pesa,nikaenda hewani,simu ikaita kidogo kisha nikasikia"simu ya mteja uliepiga inatumika" ikiashiria sim imekatwa,nikakata sim,mara kidogo nikapokea ujumbe kutoka mpenzi wangu
"nilitaka kujua kama meseji umeipata,sitaki mapenzi na wewe,futa namba yangu" nikashtuka kidogo,nikajua ni utani,kisha nikataka kujua ni ujumbe gani huo
Nikaenda inbox nikakuta ujumbe uliokua umetumwa haujasomwa ni wake akinijulisha mimi na yeye basi. Nikampigia sim hapokei,nikatuma ujumbe hakujibu. Msiba wa ndugu yangu ukawa mchungu zaidi
Siku zikaenda hivyo nikiwa siamini kilichotokea,bila ugomvi,bila sababu ya msingi nikawa nimeachwa. Nikatumia kila mbinu kumbembeleza na kumshawishi,kupitia kwa ndugu zake,marafiki zangu na ndugu zangu akagoma.
Ratiba zetu ilikua mwezi wa kumi mwaka jana nikajitambulishe rasmi,mwezi wa pili mwaka huu tufunge ndoa . Mipango hiyo ikawa imekufa. Niliyumba sana baada ya hilo tukio,nimejikaza nikasimama kiume ila kwa maumivu makali sana.
Kituko cha mwaka ni kua binti huyo kamwambia rafiki yangu kua bado ananipenda na anatamani turudiane, hadi naandika ujumbe huu huyo binti toka juzi anapiga sim(sijapokea simu yake hata moja) na kutuma ujumbe akiniomba nimsamehe
Wadau,nimrudie kisha nimtende kama alivyonifanya au nimuache aendelee na maisha yake(sina hisia nae tena na wala simpendi,,namchukia sana,natamani kisasi juu yake),ebu nishaurini wandugu.
Post a Comment