0


Mpoto akiwa uwanja wa ndege Dar es salaam akirejea toka Dubai
Mpoto ameiambia bongo5 kuwa amesemwa sana kuhusu tabia ya kuto vaa viatu lakini ameshindwa kubadilika.“Beauty yoyote ipo kwenye jicho,unapozungumzi Mrisho Mpoto kuwa peku ,sehemu nyingi sana,mara nyingi sana watu wananiona peku, ni kwa sababu ya kutafuta energy ,unajua energy ya mimi kuendelea kuishi inapatikana kwenye udongo,yani ngozi yangu inapokutana na ardhi nakuwa so (confident) na nakuwa Mpoto, zaidi na nguvu na nakuwa na akili ,sasa sipendi wakati mwingine kuwa fake,najitaidi sana kuwa wakisasa ila nakuwa nasahau,kwamfano naweza nikanunu kiatu cha gharama alafu nikakisahau kwenye ndege au kwenye basi kwasababu siyo kawaida yangu kuvaa viatu, nisha jaribu lakini nimeshapoteza vingi,kwasababu siyo culture yangu kuvaa viatu ,viatu navaaga kwasababu watu wananisema.kwaiyo nikivaa ninakuwa kama inanisumbua, nikaona kama bora niache,alafu nakuwa siko huru,ukinikuta nimevaa viatu alafu tukaanza kufanya mazungumzo nakuwa siko huru kwasababu nakuwa nipo kama naelea hewani,yani kama sina chaji,kwaiyo kwangu mimi ardhi ni kama plug ya mwili wangu,nikikanyaga chini wewe niulize chochote nitakujibu niambie niandike shairi la haina yoyote,mimi ata nikiandika nyumbani kwangu lazima niweke miguu kwenye mchanga,ata nyumbani kwangu hakuna mchanga mimi ninabeseni kabisa la michanga,kwajili tu yakukanyaga yani nikiandika nakuwa confidant ata nikiandika nakuwa na amani”Alisema MpotoPia Mrisho ataendelea kufafanua kwanini ataki kubadilika na kuchana na tamaduni ya kutembea mbila kuvaa viatu“Nataka maisha yasiniendeshe mimi,mimi niyaendeshe maisha, kwasababu unajua speed ya utandawazi yani globalization ni kubwa sana kuliko speed ya mwanadamu kwa Tanzania,ukiangalia watu kama Marekani wamepata uhuru miaka mia mbili iliyopita,sisi tuna miaka mingapi tu ya uhuru na teknologia inakuja kwa kasi sana,ndiyo maana technologia inapokuta Tanzania watu wanaimasta sana,kwamfano facebook,instargam,twetter,whatsapp na mitandao mingine vimekuja kwa kasi sana na watu vimewabadilisha sana,ata Ngugi wa Thiong’o alisema huwezi kwenda kwa jirani kama ujatokea kwako,mtu kaka mimi ninapoigia kwenye technologia siwezi badilishwa kwasababu nimeshajijua mimi ninani”Alimalizia MpotoFrom:Bongo5

Post a Comment

 
Top