Rapper Shetta alipata ajali mbaya ya gari wakati akielekea Babati, mkoani Manyara kufanya show, lakini Mungu alimnusuru yeye na watu wengine wawili aliokuwa nao katika gari hilo.
Akiongea na Times 100.5 Fm, rapper huyo amesimulia jinsi ajali
hiyo ilivyotokea ambapo ametaja chanzo cha ajali hiyo ni kumkwepa
pundamilia aliyekuwa akikatiza barabarani.
“Mi nilikuwa natoka Dar na ndege mpaka Arusha, mimi nilikuwa na show
Babati jana. Arusha mpaka Babati ni masaa mawili au matatu. Kufika
njiani kuna sehemu inaitwa Minjingo kama sikosei kuna wanyama wanyama
hapo. Tulikuta pundamilia mmoja barabarani, alikuwa ameshavuka…sasa
wakati gari pia haijavuka nae alikuwa anataka kurudi tena huko halafu
gari ilikuwa speed kidogo, sasa katika kupigapiga break ndio gari
ikapinduka.” Ameeleza Shetta.
“Gari imeumia sana lakini sisi hatukuumia hiivyo, ni maumivu tu ya
kawaida. Hapa nilipo ndio naelekea hospitali kufanya checkup ya mwili
kama kutakuwa na internal effects lakini kwa nje niko vizuri sana.”
Ameongeza Shetta.
Ameeleza kuwa ilibidi show yake iahirishwe hadi jana jumamosi kwa kuwa kila mtu alikuwa amepata taarifa kuhusu ajali hiyo.
Katika hatua nyingine, rapper huyo ameeleza kuwa alikuwepo mtu
aliyepokea pesa ya show hiyo kwa jina lake hivyo baada ya waandaaji
kwenda Dar walifanikiwa kupata namba halisi ya Shetta ambaye walimuomba
awasaidie kufanya show hiyo ili kulinda jina lao kuliko kuahirisha.
Hata hivyo, Shetta amesema tayari polisi wanamshikilia mtu aliyekuwa
amewaunganisha waandaaji hao na Shetta feki na kwamba anatamani kuongea
nae ili afahamu undani wa mchezo huo wa kitapeli.
Source: Times 100.5 fm
Post a Comment