Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira, amesema hakushangazwa na kitendo cha kutoka nje ya bunge wajumbe wa UKAWA kwani, ni matukio yaliyopangwa muda.
Wasira alisema
UKAWA walikuwa na mpango huo muda mrefu baada ya kuona hoja yao kuhusu
kutokuwepo kwa hati ya muungano kukosa ukweli.
Akizungumza na
waandishi wa habari jana, Wasira alisema sababu wanayosema kuwa
wametukanwa ndipo wakaamua kutoka nje ya bunge, haina mashiko kwani
UKAWA walitoa maneno ya kashfa dhidi ya waasisi wa Muungano.
“Hoja iliyotolewa na Kiongozi wa UKAWA kuwa wanatukanwa bungeni ni ya ajabu kwa kuwa UKAWA wamekuwa wakiwatolea maneno yasiyofaa waasisi wa muungano, kitendo ambacho hakikubaliki na Wananchi” alisema
Aliongeza kuwa ni muhimu kwa wajumbe wa bunge hilo kushindana kwa hoja na sio kutoka nje ya bunge na kutafuta sababu zisizokuwa na msingi.
Post a Comment