
Katika baadhi ya mitandao ya habari ya kijamii zimekuwepo habari zilizonukuliwa zikitoa taarifa kuwa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limetangaza nafasi za ajira kwa Wahifadhi Wanyamapori madaraja ya pili na tatu.
Shirika
la Hifadhi za Taifa linapenda kutoa ufafanuzi kuwa nafasi hizo zilizotangazwa sio za Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)
bali ni ajira zilizotangazwa na Serikali
Kuu kupitia Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma – Ofisi ya Rais
na ambako kimsingi maombi ya nafasi hizo ndiko yanakopaswa kupelekwa.
Imetolewa na Idara ya Mawasiliano
Hifadhi za Taifa Tanzania
10.04.2014
Post a Comment