0

A. TANGAZO LA NGAZI YA CHETI {TANGAZO LA STASHAHADA LIPO CHINI}

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Simu: 022-2110146/2110150/2, 211679, Faksi: 022-2113271, Tovuti: www.moe.go.tz
TANGAZO LA NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI KWA
MWAKA WA MASOMO 2014/2015
UTANGULIZI

Moja ya mikakati ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi katika kuandaa walimu
mahiri ni pamoja na kuhakikisha kuwa wanafunzi wanaochaguliwa kujiunga na
mafunzo ya ualimu ngazi ya Cheti ni wale wenye ufaulu mzuri katika mtihani ya kidato
cha NNE. Ili kufanikisha azma hii, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi itadahili
wanafunzi wenye ufaulu wa Daraja la Tatu kwa ajili ya Cheti na wenye ufaulu wa
alama 26 au 27 (mwaka 2004 hadi 2012) na alama 33 au 34 (mwaka 2013) watadahiliwa
katika programu ya mafunzo kabilishi ya mwaka mmoja.
Aidha, kipaumbele katika udahili kitatolewa kwa waombaji waliofaulu masomo ya
Sayansi, Hisabati, English na Kiswahili. Watakaojiunga na mafunzo ya ualimu na
kufaulu mafunzo yao watapatiwa ajira moja kwa moja kulingana na taratibu za Serikali.
VIGEZO
Vigezo vifuatavyo vitatumika kuchagua wanachuo wa kujiunga na mafunzo ya ualimu
mwaka 2014/15.
1:
MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA CHETI DARAJA ‘A’:
MUDA MIAKA 2
(i) Cheti Ualimu wa kawaida katika vyuo vya Ilonga, Kabanga, , Kitangali,
Mandaka , Murutunguru , Ndala , na Tarime
(ii) Cheti Ualimu Elimu ya Awali katika vyuo vya Kabanga, Kinampanda,
Mhonda, Mtwara (U), Singachini, Tandala, Tarime
(iii) Cheti Ualimu Elimu kwa michezo katika vyuo vya Ilonga, Tarime, Ndala
na Mtwara (U)
Mwombaji awe:
Mhitimu wa Kidato cha IV kati ya mwaka 2004 na 2013 mwenye ufaulu wa
kiwango kisichopungua Daraja la III katika Mtihani uliofanyika katika kikao
kimoja.
2:
MAFUNZO KABILISHI NGAZI YA CHETI (BRIDGING COURSE) KWA
AJILI YA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI:-
MUDA MWAKA 1
Mafunzo katika vyuo vya ualimu Bustani, Kinampanda, Mhonda, Mpuguso,
Mtwara (U), Nachingwea, Singachini, Tandala, Katoke na Sumbawanga
2
Mwombaji awe:
(i)
Amehitimu wa Kidato cha IV kati ya mwaka 2004 hadi 2012 na awe
amefaulu kwa kiwango kisichopungua Daraja la IV kwa alama 26 au 27
(kwa mtihani wa mwaka 2004 hadi 2012) na alama 33 au 34 (mtihani wa
mwaka 2013) kwa mitihani iliyofanyika katika kikao kimoja; na
(ii) Mwenye ufaulu wa angalau kiwango cha D katika masomo ya Sayansi,
Hisabati, English na Kiswahili katika Mtihani wa Kidato cha IV.
Tanbihi: Watakaofaulu mtihani wa mafunzo rekebishi wataendelea na
mwaka wa pili wa mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti Daraja A
3:
ELIMU MAALUM: MIAKA 2 katika chuo cha Patandi:-
Mwombaji awe:
(i) Mwalimu wa Daraja ‘A’ mwenye uzoefu wa kazi ya Ualimu kwa muda
usiopungua miaka miwili.
(ii) Mwenye ufaulu angalau somo moja la Sayansi katika Mtihani wa Kidato cha
IV.
Tanbihi:Walimu wanaofundisha Elimu Maalum hata kama hawana mafunzo
maalumu ni sifa ya nyongeza (uthibitisho uambatishwe).
MAELEZO MUHIMU
(i)
Vigezo vilivyoelekezwa kwa waombaji wa mafunzo ya Ualimu ngazi ya Cheti ni
kwa ajili ya waombaji wa mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Ualimu vya
Serikali na visivyo vya Serikali;
(ii)
Muombaji wa chuo cha ualimu cha Serikali anatakiwa kuchagua vyuo
visivyopungua vitano ambavyo angependa kujiunga navyo akianzia kile
anachokipendelea zaidi;
(iii)
Wahitimu Kidato cha IV mwaka 2013 waliojaza nafasi ya mafunzo ya Ualimu
ngazi ya Cheti Daraja ‘A’ kwenye ‘Selforms’ wakati wanamaliza Elimu ya
Sekondari wanatakiwa kuomba upya mafunzo hayo;
(iv)
Waombaji wa mafunzo ya Ualimu walioajiriwa watakaopatiwa nafasi za mafunzo
watapaswa kupata ruhusa (Release) kutoka kwa waajiri wao;
(v)
Majibu kwa watakaochaguliwa kujiunga na mafunzo ya Ualimu katika vyuo vya
Serikali yatatolewa kwenye Tovuti za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
(www.moe.go.tz),
OWM-TAMISEMI
(www.pmoralg.go.tz)
na
NACTE
(www.nacte.go.tz)
(vi)
Waombaji watakaochaguliwa watatumiwa barua za kujiunga na mafunzo na
Wakuu wa vyuo vya Ualimu watakakokuwa wamepangwa kupitia anuani zao;
(vii) Tangazo hili lipo pia katika tovuti ya OWM TAMISEMI: www.pmoralg.go.tz na
NACTE: www.nacte.go.tz na kwenye ofisi za Makatibu Tawala (M) na vyuo vya
ualimu.
Namna ya kutuma maombi:
a) Waombaji watume maombi yao kwa njia ya MTANDAO (online application) kupitia
tovuti zifuatazo: www.moe.go.tz AU www.nacte.go.tz
3
Maombi kwa njia ya mtandao yataambatana na ada ya shilingi 10,000 itakayolipwa
kwa kutumia MPESA. Maelekezo ya kina kuhusu namna ya kutuma maombi kwa
njia ya mtandao yanapatikana katika tuvuti ya wizara www.moe.go.tz na Baraza la
Taifa la Elimu ya Ufundi www.nacte.go.tz
Malipo ya maombi yanaweza kufanyika kupitia MPESA kama ifuatavyo:
1. Piga *150*00#
2. Chagua 4. (Lipa kwa MPESA);
3. Chagua 1. (Weka LIPA Namba);
4. Weka LIPA Namba (ingiza namba 607070);
5. Ingiza kiasi (ingiza kiasi cha 10,000.00);
6. Weka Enter Reference No. ( ingiza 1234);
7. Weka namba ya SIRI (ingiza namba yako ya siri); na
8. Ingiza 1 kuthibibitisha malipo.
AU
b) Barua kwa:
KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
S.L.P. 9121
DAR ES SALAAM (Aione: Mkurugenzi, Elimu ya Ualimu)
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>

B: TANGAZO LA STASHAHADA.

1
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Simu:022-2110146/2110150/2/211679 Faksi:022-2113271, Tovuti: www.moe.go.tz
TANGAZO LA NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA
STASHAHADA KWA MWAKA WA MASOMO 2014/2015
UTANGULIZI
Moja ya mikakati ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi katika kuandaa
walimu mahiri ni pamoja na kuhakikisha kuwa wanafunzi wanaochaguliwa
kujiunga na mafunzo ya ualimu ngazi ya Stashahada ni wale wenye ufaulu
mzuri katika mitihani ya kidato cha NNE na SITA. Ili kufanikisha azma hii,
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, itadahili wanafunzi wenye ufaulu wa
Daraja la Kwanza hadi Daraja la Tatu tu.
Aidha, kutokana na upungufu mkubwa wa walimu wa Sayansi na Hisabati wa
takribani walimu 26,000 kipaumbele katika udahili kitatolewa kwa waombaji
waliofaulu masomo Sayansi na Hisabati ili kuziba pengo hili. Nia ya Serikali ni
kuwavutia wanafunzi wengi wa masomo ya Sayansi na Hisabati. Kuanzia
mwaka huu wa masomo 2014/15 wanafunzi watakaojiunga na fani ya Ualimu
kwa masomo ya Sayansi na Hisabati watagharimiwa na Serikali kupitia mfumo
wa ruzuku na mkopo. Wanafunzi watakaokuwa na ufaulu wa Daraja la Kwanza
watapatiwa Ruzuku na wale wenye Daraja la Pili na la Tatu watapewa mkopo ili
kuwasaidia katika masomo yao. Watakaofaulu mafunzo ya ualimu katika
masomo ya Sayansi/Hisabati watapatiwa ajira moja kwa moja kulingana na
taratibu za serikali.
VIGEZO
Vigezo vifuatavyo vitatumika kuchagua wanachuo wa kujiunga na mafunzo ya
ualimu mwaka 2014/15.
1:
MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA STASHAHADA:
MASOMO YA SAYANSI/HISABATI NA UFUNDI: MUDA MIAKA 2.
(i)
Ualimu wa masomo ya Sayansi/Hisabati katika vyuo vya Dakawa,
Kasulu, Korogwe, Morogoro, Mpapwa, Tukuyu, Songea, Butimba,
Kleruu na Monduli
2
Mwombaji awe amehitimu:
Kidato cha VI kati ya mwaka 2004 na 2013 na awe na ufaulu wa
‘Principal Pass’ mbili katika Masomo ya Sayansi na Hisabati.
(ii)
Ualimu wa ufundi katika chuo cha ualimu Kleruu
Mwombaji awe amehitimu:
a. Mafunzo ya FTC kati ya mwaka 2004 na 2010 kutoka Vyuo vya
Ufundi, Au
b. Mafunzo ya ufundi katika ngazi ya NTA Level 6 au sifa
linganishi (equivalent qualification) kati ya mwaka 2007 na 2013
kutoka chuo chochote cha Ufundi kinachotambulika na Baraza la
Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE).
(iii) Ualimu wa Kilimo katika chuo cha ualimu Monduli
Mwombaji awe amehitimu:
Kidato cha VI kati ya mwaka 2004 na 2013 na awe na ufaulu
‘Principal Pass’ mbili katika somo la ‘Agricultural science’ na
‘Biology’, ‘Chemistry’ au ‘Food and Nutrition’.
2:
MAFUNZO MAALUM YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA
STASHAHADA KWA KIDATO CHA NNE MASOMO YA
SAYANSI/HISABATI NA ENGLISH: MUDA MIAKA 3
Ualimu wa masomo ya Sayansi/Hisabati na English katika vyuo vya
Butimba, Morogoro, Korogwe, Songea na Mpwapwa
Mwombaji awe amehitimu:
Kidato cha IV kati ya mwaka 2004 na 2013 na awe na ufaulu wa Daraja
la Kwanza hadi la Tatu, na Credit mbili (yaani A, B+, B au C) katika
masomo ya Sayansi, Hisabati na Kiingereza.
3:
MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA STASHAHADA:
MUDA MIAKA 2.
(i)
Ualimu wa masomo ya Sayansi Jamii katika vyuo vya Bunda,
Dakawa Kasulu, Korogwe, Marangu, Morogoro, Mpwapwa,
Mtwara (K), Shinyanga, Songea, Tabora, Tukuyu.
Mwombaji awe:
Amehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2004 na 2013 na awe na
ufaulu wa kiwango cha ‘Principal Pass’ mbili
3
(ii)
Biashara katika vyuo vya Shinyanga na Kasulu
Mwombaji awe:
Amehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2004 na 2013 na awe na
ufaulu wa kiwango kisichopungua ‘Principal Pass’ moja na
‘Subsidiary’ moja
(iii) Sanaa za Ufundi, Sanaa za Maonyesho, Muziki na Michezo katika
chuo cha Butimba.
Mwombaji awe:
Amehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2004 na 2013 na awe na
ufaulu wa kiwango kisichopungua ‘Principal Pass’ moja na
‘Subsidiary’ moja
Tanbihi: Masomo ya ‘Economics’, Basic Applied Mathematics’, ‘General
Studies’ na ‘Divinity’ hayatatumika kama kigezo cha kumchagua au
kumdahili mwombaji.
4:
MAFUNZO YA UALIMU TARAJALI STASHAHADA ELIMU YA
MSINGI: MUDA MIAKA 3)
Ualimu wa Stashahada ya Elimu ya Msingi katika chuo cha Vikindu
Mwombaji awe:
Amehitimu Kidato cha IV kati ya mwaka 2004 na 2013 wenye ufaulu wa
Daraja la I Daraja la Tatu katika Mtihani uliofanyika katika kikao kimoja.
Tanbihi: Kipaumbele kitatolewa kwa waombaji waliofaulu masomo ya
‘Mathematics’, ‘Biology’, ‘Physics’, ‘Chemistry’, ‘Agriculture’,
‘Food and Nutrition’, ‘English’ na Kiswahili na wahitimu
wenye mahitaji maalumu.
5.
MAFUNZO YA UALIMU KAZINI STASHAHADA:- MUDA MIAKA 2
Ualimu wa masomo ya Sayansi katika vyuo vya Dakawa, Kasulu,
Korogwe, Morogoro, Mpapwa, Tukuyu, Songea , Butimba, Kleruu na
Monduli
Mwombaji awe amehitimu:
Mwalimu wa Daraja ‘A’ aliyehitimu Kidato cha VI na mwenye ufaulu
usiopungua ‘Principal Pass’ moja na ‘Subsidiary’ moja katika Masomo ya
Sayansi na Hisabati; na mwenye uzoefu wa kazi ya Ualimu kwa muda
usiopungua miaka miwili.
4
6:
MAFUNZO YA UALIMU KAZINI STASHAHADA (SEKONDARI):-
MUDA MIAKA 2.
(i)
Ualimu wa masomo ya Sayansi Jamii katika vyuo vya Bunda,
Dakawa, Kasulu, Korogwe, Marangu, Morogoro, Mpwapwa,
Mtwara (K), Shinyanga, Songea, Tabora, Tukuyu.
Mwombaji awe:
Amehitimu Kidato cha VI kati ya mwaka 2004 na 2013 na mwenye
ufaulu usiopungua ‘Principal Pass’ moja na ‘Subsidiary’ moja
katika masomo ya ‘Biology, ‘Chemistry’ na ‘Food and Nutrition
(ii)
Ualimu wa masomo ya Biashara katika vyuo vya Shinyanga,
Kasulu
Mwombaji awe:
Mwalimu wa Daraja ‘A’ aliyehitimu Kidato cha VI na mwenye
ufaulu usiopungua ‘Principal Pass” moja na ‘Subsidiary’ moja; na
mwenye uzoefu wa kazi ya Ualimu kwa muda usiopungua miaka
miwili.
(iii) Ualimu wa masomo ya Elimu Maalumu katika chuo cha Patandi
Mwombaji awe:
Mwalimu mwenye Stashahada ya Ualimu fani ya Sayansi; Au Sayansi ya
Jamii na uzoefu wa kazi ya ualimu kwa muda usiopungua miaka miwili,
Au
Mwalimu wa Daraja ‘A’ aliyehitimu Kidato cha VI na mwenye ufaulu
usiopungua ‘Principal Pass’ moja na ‘Subsidiary’ moja; na mwenye
uzoefu wa kazi ya Ualimu kwa muda usiopungua miaka miwili.
Tanbihi: Walimu wanaofundisha watoto wenye mahitaji maalum kama
wasioona, viziwi, wenye ulemavu wa akili, n.k. ni sifa ya nyongeza
(vithibitisho viambatishwe).
7:
MAFUNZO YA UALIMU KAZINI STASHAHADA ELIMU YA
MSINGI: MUDA MIAKA 2:
Ualimu wa Stashahada ya Elimu ya Msingi katika chuo cha Vikindu
Mwombaji awe:
Mwalimu wa Daraja ‘A’ mwenye uzoefu wa kazi ya Ualimu kwa muda
usiopungua miaka miwili.
5
MAELEZO MUHIMU
(i)
Vigezo vilivyoelekezwa kwa waombaji wa mafunzo ya Ualimu ngazi ya
Stashahada ni kwa ajili ya waombaji wa mafunzo ya Ualimu katika Vyuo
vya Ualimu vya Serikali na visivyo vya Serikali;
(ii)
Muombaji wa chuo cha ualimu cha Serikali anatatakiwa kuchagua vyuo
visivyopungua vitano ambavyo angependa kujiunga navyo akianzia kile
anachokipendelea zaidi;
(iii)
Waombaji wa mafunzo ya Ualimu walioajiriwa watakaopatiwa nafasi za
mafunzo watapaswa kupata ruhusa (Release) kutoka kwa waajiri wao;
(iv)
Majibu kwa watakaochaguliwa kujiunga na mafunzo ya Ualimu katika
vyuo vya Serikali yatatolewa kwenye Tovuti za Wizara ya Elimu na
Mafunzo
ya
Ufundi
(www.moe.go.tz),
OWM-TAMISEMI
(www.pmoralg.go.tz) na NACTE (www.nacte.go.tz)
(v)
Waombaji watakaochaguliwa watatumiwa barua za kujiunga na mafunzo
na Wakuu wa vyuo vya Ualimu watakakokuwa wamepangwa kupitia
anuani zao;
(vi)
Tangazo
hili
lipo
pia
katika
tovuti
ya
OWM
TAMISEMI:
www.pmoralg.go.tz na NACTE: www.nacte.go.tz na kwenye ofisi za
Makatibu Tawala (M) na vyuo vya ualimu.
Namna ya kutuma maombi:
a) Waombaji watume maombi yao kwa njia ya MTANDAO (online application)
kupitia tovuti zifuatazo: www.moe.go.tz AU www.nacte.go.tz
Maombi kwa njia ya mtandao yataambatana na ada ya shilingi 10,000
itakayolipwa kwa kutumia MPESA. Maelekezo ya kina kuhusu namna ya
kutuma maombi kwa njia ya mtandao yanapatikana katika tuvuti ya wizara
www.moe.go.tz na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi www.nacte.go.tz
Malipo ya maombi yanaweza kufanyika kupitia MPESA kama ifuatavyo:
1. Piga *150*00#
2. Chagua 4. (Lipa kwa MPESA);
3. Chagua 1. (Weka LIPA Namba);
4. Weka LIPA Namba (ingiza namba 607070);
5. Ingiza kiasi (ingiza kiasi cha 10,000.00);
6. Weka Enter Reference No. ( ingiza 1234);
7. Weka namba ya SIRI (ingiza namba yako ya siri); na
8. Ingiza 1 kuthibibitisha malipo.
AU
6
b) Barua kwa:
KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
S.L.P. 9121
DAR ES SALAAM (Aione: Mkurugenzi, Elimu ya Ualimu)

CHANZO: TOVUTI YA WIZARA YA ELIMU

Post a Comment

 
Top