Ofisa wa polisi mwenye cheo cha Koplo, Wilson Mwakipesile wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani Kilimanjaro amefariki dunia ghafla akiwa ndani ya daladala alilokuwa amelikamata.
Hata hivyo, haikujulikana mara moja iwapo trafiki
huyo alifariki dunia akiwa njiani kulipeleka gari hilo kituo cha polisi,
alifariki muda mfupi baada ya kufika kituoni au wakati anapelekwa
hospitali.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz
alisema polisi huyo alikufa ghafla akiwa kazini lakini alikataa kuingia
kwa undani wa tukio hilo lilitokea Ijumaa kati ya saa 5:00 asubuhi na
saa 6:00 mchana, baada ya trafiki huyo kukamata daladala linalofanya
kazi zake kati ya Kiborloni na katikati ya mji.
Mmoja wa mashuhuda alisema :“Baada ya kuikamata
hiyo Hiace (Toyota) pale Kiborloni aliingia kwenye hiyo gari na kukaa
kiti cha mbele pembeni ya dereva na kumwamuru kulipeleka kituoni.
“Wakati wakiwa njiani kuelekea kituoni ghafla yule
trafiki akawa haongei na akawa anamwegemea dereva… hiyo hali iliendelea
hadi walipofika kituoni ndipo dereva akawaeleza trafiki wenzake.”
Mwili wa polisi huyo ulisafirishwa juzi kwenda Mbeya kwa mazishi.
Mwili wa polisi huyo ulisafirishwa juzi kwenda Mbeya kwa mazishi.
Post a Comment