ALFAJIRI ya Alhamisi ya wiki iliyopita haitasahaulika kwa wakazi wa
Jiji la Dar es Salaam na viunga vyake ambapo maafa makubwa yalipoanza
kufuatia mafuriko ya mvua zilizonyesha mfululizo na kusababisha vifo na
uharibifu wa mali hivyo kuonesha wazi kuwa, kumbe Dar si salama.
Daraja linalounganisha wilaya ya Bagamoyo na Mkoa wa Dar es Salaam likiwa limekatika baada ya mvua kubwa kunyesha.
Idadi ya vifo iliyoripotiwa mpaka juzi jioni ni kumi na mbili huku
wanachi wengi wakikosa makazi na wengine kupotea kwa kusombwa na
mafuriko.
UWAZI MZIGONI
Timu ya Uwazi ilizunguka sehemu tofauti za jiji zilizozizima na kushuhudia maafa hayo.
Tukio la kwanza ni kuonekana laivu kwa maiti ya mtu mmoja aliyezolewa
na maji maeneo ya Jangwani wilayani Ilala.Mbali na kushuhudia uharibifu
wa kutisha wa miundombinu na mateso ya watu walioathirika.
![](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_sAN2aq8bdUNhASv1O79009qWmt-Z__fg0hd4hvNrmA-10LD4lsQcfUMy_hpiGB6gKKqWrnJysgg93JnvIwagfPn-S4bt0ojHC79oHXonS_ukInxfwFIpeJ3yPWeOyXypMHq5R11fbwtopVqb67w04lvi5BAaikfGvIIJ0UZJH4dyMOO3gEPv8LQbsEEsFZhqGQEqsKVi_jgjoRMS-blv93EHlPYydHKOIlBz9QzslIEwbJ4Ive=s0-d)
Helkopta ya Jeshi la Wananchi iliyokuwa imebeba viongozi wa serikali ikiwa imeanguka baada ya kupoteza mwelekeo.
BARABARA ZAFUNGWA, MADARAJA YAZOLEWA
Uwazi lilishuhudia baadhi ya barabara zikiwa zimefungwa kufuatia kujaa
maji na madaraja kuvunjika na mengine kuzolewa. Barabara zilizofungwa ni
pamoja na Dar es Salaam – Pwani kwa daraja la Mto Mpiji kubomoka.
Pia Barabara ya Dar- Kibiti ilifungwa na kufanya magari ya kwenda Kusini kutofanya safari kwa siku ya Jumapili iliyopita.
Daraja
la Mto Ruvu lilifungwa kutokana na maji kupita juu ya daraja hivyo
kufanya usafiri wa kutoka Dar kwenda mikoani kuwa mgumu sanjari na
kuingia jijini Dar.
MADARAJA YAFUNIKWA
Ndani ya Jiji la Dar madaraja
mengi yalijaa maji ikiwa ni pamoja la Kinyerezi, Mlalakua, Mpiji Magoe
kwenda Kidimu, Mbezi Mwisho, Msewe Kimara, Kijichi na Jangwani.
WAKAZI WAKOSA PA KUKAA
Baadhi ya maeneo ya jiji hasa Kigogo, Mwananyamala, Jangwani, Tandale,
Mabibo na Tabata yalikumbwa na kadhia ya maji kujaa kwenye makazi ya
watu na kusababisha wakazi wake kukaa kwenye mapaa kusubiri kuokolewa.
WAZEE, WATOTO, WANAWAKE WAKATI MGUMU
Makundi yaliyoonekana kupata wakati mgumu kwa mafuriko hayo ni wazee,
wanawake na watoto waliokuwa wakishindwa kupanda juu ya mapaa ya nyumba,
hivyo kusimama kwa kubebana kwenye maji kwa muda mrefu, waliopata
bahati waliokolewa na watu wenye nguvu wakiwemo vijana.
MAITI, MAJERUHI WAKIMBIZWA HOSPITALI
Uwazi lilishuhudia miili ikipelekwa Hospitali ya Taifa Mubimbili kwa hifadhi huku ikiwa na dalili ya kuharibika.
Idadi kubwa ya majeruhi ambao hali zao zilikuwa mbaya walikimbizwa katika Hospitali za Amana, Mwananyamala na Temeke.
MAENEO HATARI ZAIDI
Maeneo mengi jijini
yameathirika, lakini ambayo hayako salama kabisa ni mabondeni kama
Jangwani, Kigogo Sambusa, Tabata ya Matumbi, Mikocheni na Msasani.
KOVA, MKUU WA MKOA WAPATA AJALI
Jumapili
asubuhi, Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova
akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadik walipata ajali
ya chopa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ‘JNIA’
walipokuwa wakijiandaa kwenda kutembelea sehemu zenye mafuriko.
DAR SI SALAMA
Imebainika kuwa, miundombinu ya maji jijini Dar ndiyo sababu ya kutokea
kwa mafuriko makubwa kwa vile maji hukosa njia ya kupita na kutengeneza
visiwa vidogovidogo kila mahali.
“Kama mnavyoona Dar si salama, iko siku jiji lote litafunikwa na
maji. Mvua kidogo mafuriko, watu wanakufa. Yaani vifovifo njenje,”
alisema mkazi mmoja wa Mwananyamala Kisiwani baada ya kunusurika na
mafuriko.
WATAALAM WANENA
Wataalam mbalimbali wa masuala
ya mabadiliko ya tabianchi wamebainisha kasoro kubwa katika mipango miji
nchini kwamba haizingatii madhara yatokanayo na mabadiliko ya hali ya
hewa na kuruhusu ujenzi holela mabondeni, milimani na kwenye mikondo ya
maji, ikiwemo mifereji.
“Hatua ya kuruhusu makazi kwenye maeneo ya mabondeni na kwenye mapito
ya maji huzuia mikondo ya maji hivyo mvua zinaponyesha maji yake
hulazimisha njia na matokeo yake ni mafuriko yenye madhara makubwa kwa
maisha ya watu na mali zao,” alisema mtaalam mmoja kutoka Mamlaka ya
Hali ya Hewa Tanzania ‘TMA’ huku akiomba hifadhi ya jina lake.
SERIKALI KUENDELEA KUGHARAMIA MADARAJA
Kwa
mujibu wa mtaalam huyo, ujenzi wa barabara na madaraja nchini pia
hauzingatii suala la mabadiliko ya tabianchi ambalo ni ajenda kuu kwa
sasa duniani na ndiyo maana mvua nyingi Tanzania hubomoa madaraja na
barabara na kuigharimu serikali mabilioni ya fedha kwa ajili ya
ukarabati.
ALFAJIRI ya Alhamisi ya wiki iliyopita haitasahaulika kwa wakazi wa
Jiji la Dar es Salaam na viunga vyake ambapo maafa makubwa yalipoanza
kufuatia mafuriko ya mvua zilizonyesha mfululizo na kusababisha vifo na
uharibifu wa mali hivyo kuonesha wazi kuwa, kumbe Dar si salama.
Daraja linalounganisha wilaya ya Bagamoyo na Mkoa wa Dar es Salaam likiwa limekatika baada ya mvua kubwa kunyesha.
Idadi ya vifo iliyoripotiwa mpaka juzi jioni ni kumi na mbili huku
wanachi wengi wakikosa makazi na wengine kupotea kwa kusombwa na
mafuriko.
UWAZI MZIGONI
Timu ya Uwazi ilizunguka sehemu tofauti za jiji zilizozizima na kushuhudia maafa hayo.
Tukio la kwanza ni kuonekana laivu kwa maiti ya mtu mmoja aliyezolewa na maji maeneo ya Jangwani wilayani Ilala.Mbali na kushuhudia uharibifu wa kutisha wa miundombinu na mateso ya watu walioathirika.
![](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_sAN2aq8bdUNhASv1O79009qWmt-Z__fg0hd4hvNrmA-10LD4lsQcfUMy_hpiGB6gKKqWrnJysgg93JnvIwagfPn-S4bt0ojHC79oHXonS_ukInxfwFIpeJ3yPWeOyXypMHq5R11fbwtopVqb67w04lvi5BAaikfGvIIJ0UZJH4dyMOO3gEPv8LQbsEEsFZhqGQEqsKVi_jgjoRMS-blv93EHlPYydHKOIlBz9QzslIEwbJ4Ive=s0-d)
Uwazi lilishuhudia baadhi ya barabara zikiwa zimefungwa kufuatia kujaa maji na madaraja kuvunjika na mengine kuzolewa. Barabara zilizofungwa ni pamoja na Dar es Salaam – Pwani kwa daraja la Mto Mpiji kubomoka.
Pia Barabara ya Dar- Kibiti ilifungwa na kufanya magari ya kwenda Kusini kutofanya safari kwa siku ya Jumapili iliyopita.
Daraja
la Mto Ruvu lilifungwa kutokana na maji kupita juu ya daraja hivyo
kufanya usafiri wa kutoka Dar kwenda mikoani kuwa mgumu sanjari na
kuingia jijini Dar.
MADARAJA YAFUNIKWA
Ndani ya Jiji la Dar madaraja mengi yalijaa maji ikiwa ni pamoja la Kinyerezi, Mlalakua, Mpiji Magoe kwenda Kidimu, Mbezi Mwisho, Msewe Kimara, Kijichi na Jangwani.
WAKAZI WAKOSA PA KUKAA
Baadhi ya maeneo ya jiji hasa Kigogo, Mwananyamala, Jangwani, Tandale, Mabibo na Tabata yalikumbwa na kadhia ya maji kujaa kwenye makazi ya watu na kusababisha wakazi wake kukaa kwenye mapaa kusubiri kuokolewa.
WAZEE, WATOTO, WANAWAKE WAKATI MGUMU
Makundi yaliyoonekana kupata wakati mgumu kwa mafuriko hayo ni wazee, wanawake na watoto waliokuwa wakishindwa kupanda juu ya mapaa ya nyumba, hivyo kusimama kwa kubebana kwenye maji kwa muda mrefu, waliopata bahati waliokolewa na watu wenye nguvu wakiwemo vijana.
MAITI, MAJERUHI WAKIMBIZWA HOSPITALI
Uwazi lilishuhudia miili ikipelekwa Hospitali ya Taifa Mubimbili kwa hifadhi huku ikiwa na dalili ya kuharibika.
Idadi kubwa ya majeruhi ambao hali zao zilikuwa mbaya walikimbizwa katika Hospitali za Amana, Mwananyamala na Temeke.
MAENEO HATARI ZAIDI
Maeneo mengi jijini yameathirika, lakini ambayo hayako salama kabisa ni mabondeni kama Jangwani, Kigogo Sambusa, Tabata ya Matumbi, Mikocheni na Msasani.
KOVA, MKUU WA MKOA WAPATA AJALI
Jumapili asubuhi, Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadik walipata ajali ya chopa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ‘JNIA’ walipokuwa wakijiandaa kwenda kutembelea sehemu zenye mafuriko.
DAR SI SALAMA
Imebainika kuwa, miundombinu ya maji jijini Dar ndiyo sababu ya kutokea kwa mafuriko makubwa kwa vile maji hukosa njia ya kupita na kutengeneza visiwa vidogovidogo kila mahali.
“Kama mnavyoona Dar si salama, iko siku jiji lote litafunikwa na maji. Mvua kidogo mafuriko, watu wanakufa. Yaani vifovifo njenje,” alisema mkazi mmoja wa Mwananyamala Kisiwani baada ya kunusurika na mafuriko.
WATAALAM WANENA
Wataalam mbalimbali wa masuala ya mabadiliko ya tabianchi wamebainisha kasoro kubwa katika mipango miji nchini kwamba haizingatii madhara yatokanayo na mabadiliko ya hali ya hewa na kuruhusu ujenzi holela mabondeni, milimani na kwenye mikondo ya maji, ikiwemo mifereji.
“Hatua ya kuruhusu makazi kwenye maeneo ya mabondeni na kwenye mapito ya maji huzuia mikondo ya maji hivyo mvua zinaponyesha maji yake hulazimisha njia na matokeo yake ni mafuriko yenye madhara makubwa kwa maisha ya watu na mali zao,” alisema mtaalam mmoja kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania ‘TMA’ huku akiomba hifadhi ya jina lake.
SERIKALI KUENDELEA KUGHARAMIA MADARAJA
Kwa mujibu wa mtaalam huyo, ujenzi wa barabara na madaraja nchini pia hauzingatii suala la mabadiliko ya tabianchi ambalo ni ajenda kuu kwa sasa duniani na ndiyo maana mvua nyingi Tanzania hubomoa madaraja na barabara na kuigharimu serikali mabilioni ya fedha kwa ajili ya ukarabati.
UWAZI MZIGONI
Timu ya Uwazi ilizunguka sehemu tofauti za jiji zilizozizima na kushuhudia maafa hayo.
Tukio la kwanza ni kuonekana laivu kwa maiti ya mtu mmoja aliyezolewa na maji maeneo ya Jangwani wilayani Ilala.Mbali na kushuhudia uharibifu wa kutisha wa miundombinu na mateso ya watu walioathirika.
Helkopta ya Jeshi la Wananchi iliyokuwa imebeba viongozi wa serikali ikiwa imeanguka baada ya kupoteza mwelekeo.
BARABARA ZAFUNGWA, MADARAJA YAZOLEWAUwazi lilishuhudia baadhi ya barabara zikiwa zimefungwa kufuatia kujaa maji na madaraja kuvunjika na mengine kuzolewa. Barabara zilizofungwa ni pamoja na Dar es Salaam – Pwani kwa daraja la Mto Mpiji kubomoka.

Post a Comment