Miili ya watu wapata 350 imepatikana
hapo jana katika maporomoko ya ardhi kazkazini mashariki mwa taifa hilo
na hakuna mtu yoyote aliyepatikana akiwa hai.Umoja wa Mataifa unasema
karibu watu 4000 hawana makazi.
Mvua kubwa zilizonyesha zimesababisha mafuriko na madhara makubwa
Baadhi walipanda kwenye paa kusubiri msaada wa uokoaji
Mashirika ya misaada na uokoaji kwa sasa
wameanza kuwapa mikate na maji maelfu ya watu waliolala nje kwenye
baridi kali wakiwa hawana makazi.
"Taarifa
zinasema ardhi na matope yameendelea kuporomoka ambapo wengi ya
waliokufa ni waokoaji ambao walikwenda kutoa msaada kwa wenzao."
Kuna taarifa nyingine zinazosema maelfu mengine
ya watu huenda wakawa wametoweka baada ya upande mmoja wa mlima
kuangukia kijiji k katika eneo la mashambani la mkoa wa Badakhshan
unaopakana na mataifa ya Tajikistan,Uchina na pakistan.
Waokoaji wamekuwa wakilalamika kuwa hawana vifaa vya kutosha kuwasaka manusura.
Mwandishi wa BBC mjini kabul anasema kuwa eneo
hilo ni miongoni mwa maeneo yenye umaskini mkubwa na katika taifa
maskini duniani na huenda ikachukua majuma kadhaa kabla ya serikali
kubaini ukubwa wa janga hilo.
BBC SWAHILI
Post a Comment