NYOTA
wa sinema za Bongo asiyetabirika maisha, Aunt Ezekiel amedaiwa kudai
talaka kutoka kwa ndugu wa mumewe Sunday Demonte kufuatia madai kwamba
alikasirishwa na manenomaneno yao kwenye vyombo vya habari.
Ntaa wa sinema za Bongo asiyetabirika maisha, Aunt EzekielKwa mujibu wa chanzo, nyota huyo aliyasema hayo mwishoni mwa wiki
iliyopita jijini Dar baada ya kutua toka Dubai alikodai alikwenda kwa
mume wake.
Ilidaiwa kwamba, mara baada ya kutua Bongo, Aunt alikutana na shoga
yake mmoja ambaye jina lake halikupatikana mara moja na kutonywa kuwa
kuna gazeti liliandika habari yake kwamba wakati mumewe akidaiwa kuwa
jela, yeye anaponda raha Dubai.
“Aunt aliambiwa kuwa wasemaji wakubwa wa maneno hayo ni ndugu wa
mumewe yaani mashemeji na mawifi zake. Wao wamesema watawasiliana na
mume wake kule aliko, hata kama ni gerezani, atoe kibali cha ndugu
yeyote wa kiume kuandika talaka na kukabidhiwa Aunt kwa vile hana
uchungu na matatizo ya mumewe.
AUNT ASHTUKA KWA MANENO YA NDUGU WA MUME
“Taarifa hizo zilimshtua
sana Aunt mpaka akaonekana kupaniki, akajibu mapigo kwa kusema ‘niko
tayari kwa talaka, kwanza mimi mwenyewe ndiyo naomba wanipe talaka. Kama
hao ndugu wanaweza kwenda kwa Demonte wakapewa kibali cha kunipa talaka
basi mimi nasema naomba wanipe’ niko tayari,” kilisema chanzo hicho
kikimkariri shoga wa Aunt.
Staa wa sinema Aunt Ezekiel akiwa na mumewe wakati wa ndoa yaoSHUTUMA NYINGINE KWA AUNT
Ama kweli ndoa ndoano, Aunt amekuwa
akitupiwa shutuma kibao kutoka kwa baadhi ya ndugu wa mumewe (baadhi
lakini) kwamba mke huyo wa ndugu yao hana ushirikiano na wanafamilia
kama vile kuwatembelea, kuwajulia hali na hata kuwatupia chochote kitu
pale anapokuwa amepata.
“Aunt tangu ameolewa mwaka juzi hajawahi kuja kwangu, mimi namwona
kwenye filamu tu. Sijui ni kwa nini Demonte alimuona anafaa kuwa mke
wake. Lakini kwa vile kupenda ni moyo, sina usemi,” alisema ndugu huyo
ambaye aliomba asichorwe gazetini.
AUNT ASAKWA
Juzi, Amani lilimtafuta Aunt kwa njia ya simu yake ya
mkononi ili ajibu madai hayo lakini hakupatikana hewani.Baadhi ya watu
wake wa karibu waliliambia gazeti hili kwamba Aunt huwa hapatikani
kwenye simu kuanzia saa kumi alfajiri hadi mchana unaofuatia kwa sababu
akisharudi nyumbani na kulala huamka mchana jua likiwa utosini.
Mapaparazi wetu walifunga safari hadi nyumbani kwake Mwananyamala na
kuambiwa hakuwepo na msichana aliyekutwa kwenye makazi hayo.
Amani: Hayupo kasafiri au?
Msichana: Hayupo tu!
Amani: Kuwa muwazi basi.
Msichana: Kwani kusema Aunt hayupo ni usiri?
Baada ya waandishi
wetu kuondoka, ilibainika kwamba Aunt ana tabia ya kulala nje, kama si
kwa staa mwenzake Wema Sepetu (Mwananyamala, Dar) basi kwa shoga yake
kipenzi, Nice Chande (Changanyikeni, Dar).
Amani lilimwendea hewani kwa njia ya simu yake ya mkononi lakini iliita kwa muda bila kupokelewa. Ilikuwa saa 9:25 alasiri.
Baada ya dakika tano, Amani lilimpigia tena ambapo alipokea. Baada ya salamu, madai yakaanza.
Amani: Inasemekana umedai talaka kutoka kwa mume wako baada ya kusikia
manenomaneno kutoka kwa mashemeji zako halafu swali jingine…
Aunt: Sitaki jamani sitaki. Ndoa yangu naomba ipumzishwe. Kwanza
naomba kusema kwamba, mimi sijasema kama nimepewa talaka au sijapewa. Ni
uamuzi wangu kusema.
“Kwa sasa sijasema lolote, siku nikitaka
nitasema. Kwani mimi ndiyo nitakuwa wa kwanza kupewa talaka? Hebu
nipumzisheni. Andikeni kuhusu filamu zangu.”
Amani: Filamu yako ipo?
Aunt: Siku ikitoka.
Amani: Basi siku ikitoka tuambie tutaandika.
Aunt: Siyo lazima niwaambie, nyie wenyewe mtaona imetoka
SOURCE: GPL
Post a Comment