0


Msanii wa muziki na producer wa Sharobaro Record, Bob Junior amekanusha habari zilizoandikwa na gazeti moja  la udaku kuwa anamloga Diamond.

Amesema hawezi Kufanya kitu kama hicho na Diamond atabaki kama Diamond na yeye kama yeye.
 
“Niupu…vu kuandika kitu kama hicho, nani mambo ya ki..nge,mimi nimekasirika sana,huwezi andika kitu kama hicho. Hivi mimi naweza nikamloga Diamond,unajua Diamond atabaki kuwa Diamond na Bob Junior atabaki kama Bob Junior,huu wote ni uongo tu,sipendi kuyaongelea haya mambo na sina tatizo na mtu yoyote,” amesema.
 
Pia Bob Junior alizungumzia tuhuma za kuhusisha muziki wake na waganga wa kienyeji.
 
“Sijawai kujihusisha na masuala ya waganga,mimi nimelelewa katika familia ambayo hata simjui mganga. Nashukuru Mungu toka nimezaliwa mpaka hapa. Sehemu kubwa yaani nasaidiwa na wazazi wangu vizuri mpaka ikafika wakati najitegemea mwenyewe. Kwahiyo sijui chochote kuhusu suala la mganga.”

Post a Comment

 
Top