Kama ulikuwa ukifikiria kuwa ugomvi katika mahusiano ni jambo baya basi
umekosea sana! Kama ukikutana na wanandoa wakakuambia hawakuwahi
kugombana au kutofautiana katika ndoa yao, ama wanakutania tu au wape
pole! Ugomvi katika mahusiano una maana zifuatazo;
UGOMVI UNA MAANA MNAPENDANA
Wanasaikolojia Bruce na John katika kitabu chao cha Language of love,
wanasema, kama wawili wanapendana kweli, lazima wagombane! Wanagombana
kwa sababu kila mmoja anatetea sehemu ya pili isiende pengine,
anailinda, anaionea wivu. Hivyo kugombana na pengine kugombezwa ni
ushahidi kuwa ndani yenu mnahitajiana na mnapendana kwa hiari.
....
UGOMVI HUTIBU MATATIZO YA HISIA (HEALTHIER EMOTIONS)
Wanandoa/Wachumba wasiotofautiana na kugombana mara kadhaa basi ni wazi
hisia za kimapenzi baina yao zinaumwa! Hapo kuna misongo ya mawazo, kuna
kulimbikiza maudhi sio upole huo, kuna hasira inayosubiri kulipuka..
Upendo wenye afya huonekana kwa hisia za wazi.
....
KUGOMBANA NI KUONESHA KUJALI (CARE)
Hapa ntatofautiana wengi wanaofikiri kuwa kumjali mwenza ni kumtoa out,
kumpa maua, kumnyoshea shati, kumpa zawadi, surprise n.k Kugombana ni
zawadi ambayo wanandoa vijana wengi hawaijui uzuri wake. Kuwa na
mahusiano yaliyopoa kabisa kuna gharama zake, wengi hushituka mambo
yalishaharibika. Mwanasaikolojia George R. Bach na Peter Wyden katika
kitabu chao cha 'How to fight fair in love' wanasema '...we have
discovered that couples who fight together are couples who stay
together- provided they know how to fight properly..."
....
Ugomvi wa wachumba huhusu zaidi mavazi, simu, mwonekano, hitaji la watoto,namna ya kutumia starehe n.k
Ugomvi wa wanandoa wengi huhusu zaidi pesa, watoto, wakwe, ndugu, majukumu, tendo la ndoa n.k
Ugomvi wa wanandoa wazee huhusu wajukuu, watoto wao wakubwa, ibaada n.k
....
TAHADHARI
Sijaruhusu kupigana makonde, unaweza kupigana na mwenza kwa kutumia
akili nyingi pasipo kutumia nguvu nyingi. Ugomvi mzuri ni ule unaoleta
suluhu mapema na usipigane kuwapa wengine faida.
Be brave
Post a Comment