MSANII wa sinema Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’ aliyewahi kutamba na filamu za kidunia, sasa ameamua kuimba muziki wa Injili ikiwa ni kumtukuza Mungu na kujiandalia maisha mema ya peponi.
Akipiga stori na mwandishi wetu juzi, staa huyo aliyekuwa akiitwa
Mwanaidi na kubadili jina baada ya kuokoka, alisema: Vijana siku zote
tuna nguvu, tuna muda wa kutosha hivyo tunapaswa kumtumikia Mungu siyo
mpaka tuchoke, tuzeeke au tufanye kwanza dhambi ikifika omega (mwisho)
ndiyo unamkumbuka Mungu.
“Ninaimba kwaya tena sauti ya tatu, subirini muone ujio wangu mpya kwani nimeamua kumtukuza Mungu aliyeumba mbingu na nchi.”
“Ninaimba kwaya tena sauti ya tatu, subirini muone ujio wangu mpya kwani nimeamua kumtukuza Mungu aliyeumba mbingu na nchi.”
Post a Comment