Wastara akivishwa pete ya uchumba
From London With Love ...!!! Star mkubwa wa filamu nchini Tanzania Wastara Juma ambaye kwasasa yupo London Uingereza amevishwa pete ya uchumba huko na mwanaume anayeonekana hapo pichani. Wastara aliweka picha kadhaa kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii na wengine kudhani ni filamu mpya. Star mwenzake pia Riyama Ally ambaye wapo wote huko London nae aliandika "Ama kweli Mungu akitaka kukupa haandiki barua......, kila la kheri mama huu mwanzo mzuri kwako".
ilimuendea hewani Wastara akiwa huko huko London na kumuuliza kama ni movie au ni kweli, tofauti na siku zote ambapo kama ni movie Star huyo huweka kweupe lakini safari hii alionekana hana la kusema pengine kwa furaha na kuishia kujibu kwa ufupi kwa kusema "No comment" alipododoswa tena alijibu hivyo hivyo tena "No comment".
Wastara Monalisa, Riyama Ally na Cloud ni takribani wiki tatu sasa wapo London kwa mwaliko maalum na kucheza filamu inayoitwa Ughaibuni(Abroad) ambapo tayari wameanza kuishuti. Tungependa kuwatakia kila la kheri wawili hao .Angalia picha zaidi Wastara akivishwa pete hiyo..............
Post a Comment