STAA mkongwe wa filamu Bongo, Suzan Lewis ‘Natasha’ ameongeza listi ya mastaa ambao wameathirika na ugonjwa wa dengue (Dengue Fever).
Akiongea na mwandishi wetu, Natasha alisema tangu Rais Jakaya
Kikwete aingie madarakani, hajawahi kuugua hata homa lakini kwa mara ya
kwanza mwaka huu homa ya dengue imemlaza.
“Nilianza kusikia baridi kali sana kisha nikawa naishiwa nguvu na
mishipa inakakamaa, nilihisi naaga dunia kiukweli lakini niliwahi kwenda
hospitali, nimepata tiba, nimeruhusiwa na ninaendelea vizuri,” alisema
Natasha.
Miongoni mwa mastaa ambao wameumwa ugonjwa huo ambao hauna tiba ya
moja kwa moja ni Rehema Chalamila ‘Ray C’, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ na
Miss Afrika Mashariki namba 2, 2008, Aneth John
Post a Comment