0

Marehemu Rashid Chilangwa, Mtunza Bustani Mkuu wa Ikulu enzi za uhai wake. Marehemu alifariki dunia siku ya sherehe za Mei Mosi katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa pole kwa wafiwa nyumbani kwa marehemu Mabibo jijini Dar es salaam.
Mama Salma Kikwete akijumuika na wafiwa katika kuomboleza msiba nyumbani kwa marehemu Rashidi Chilangwa huko Mabibo, jijini Dar es salaam.
Viongozi wa ofisi ya Rais Ikulu wakijadiliana na wanafamilia ya marehemu kuhusu mwenendo wa mazishi.
Mwili wa marehemu ukiombewa kabla ya kupelekwa shambani kwake Kisarawe kwa mazishi.
Katibu Mkuu Ikulu Mhe. Peter Ilomo akizungumza machache wakati wa msiba wa Mtunza Bustani mkuu marehemu Rashidi Chilangwa.
Mwili wa marehemu ukipakiwa kwenye gari tayari kwa safari yake ya mwisho  shambani kwake Kisarawe kwa mazishi.

Post a Comment

 
Top