0
Anaitwa Fid Q mzee wa Mwanza Mwanza anakubalika sana kwa kua mkali wa mashairi yenye vina na yanayofanya mtu afikirie sana ili kuja kumwelewa. .Baada ya ukame wa tuzo hatimaye mwaka huu alichukua tuzo ya mwaka ya msanii bora wa  HipHop katika tuzo za KTMA na akafanikiwa kua moja kati ya wasanii wachache walioshinda tuzo hizo mwaka huu na  kuchaguliwa kujiunga na Kill Tour ambayo itazunguka mikoa  ambalimbali.
Fid-Q-Kilimanjaro-Music-Awards-Vibe-co-tz
 Jumamosi iliyoisha ilikua zamu ya wakazi wa Mwanza kupata shangwe za Kill Tour na baadhi ya wasanii waliodondosha show ya nguvu ni Vanessa Mdee, Weusi, Ben Pol na Fid mwenyewe. Wasanii wengine wote walipiga show vizuri tatizo lilikuja pale alipopanda Fid-q  jukwaani.Burudani aliyotoa sio ile wakazi wa Mwanza waliyotarajia inadaiwa kua Fid Q alikua amelewa sana. Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichokua backstage kilisema kua kulikua na bia za bure zilizokua zikitolewa kwa wasanii na kampuni ya bia ya Kilimanjaro ndizo zilidaiwa kua chanzo cha Fid-q kuharibu stejini.

Chanzo hicho kiliendelea kusema kua pamoja na kutoa burudani mbaya lakini alikua akiyumba yumba na kutaka kudondoka. Mwisho wa siku alishuka lakini watu walibaki wakilalamika. Mashabiki wake hawakuridhika wakamfuata Insta na kulalamika na haya ni baadhi ya maoni :-
salumusaid broo mi nakukubal san ila jana sijafurahia shoo ata kidogo
erickhenry773 Ukaamua kuwa ahmada jana underperfomance kichz
Baada ya kuona watu wamemind sana Fid Q aliamua kufunguka na kusema haya kuhusu kufanya kwake vibaya ”Afya ilileta mgogoro.. Nxt time kama vp.. Pole kwa usumbufu uliojitokeza “

Post a Comment

 
Top