Baada ya diamond kuachia nyimbo yake ya Mdogomdogo mapema wiki hii,
hit single iliyopokelewa vizuri sana na watanzania wengi, huku kila
mmoja akiwa anasubiria kwa hamu jinsi video ya wimbo huo utakavyokuwa,
kwa mujibu wa Diamond Platnumz mwenyewe anasema, wimbo huo ni kwa ajili
ya wa tzee kwanza, ila homa ya jiji na ya bara zima la africa inakuja
mapema wiki ijayo.
Diamond Platnumz ameanza kuwa na utaratibu mpya unaomfanya atoe
nyimbo mbili kwa pamoja, ya kwanza ikiwa kwa ajili ya watzee, na kama
fans wa nchi nyingine hawataielewa, basi kuna nyingine inayotoka hivi
karibuni kwa ajili ya bara zima, hii ni kutokana na staili tofauti
anazotumia kuwakosha nyoyo mashabiki wake wa kila pande za dunia. Sauti
ya Iyanya ndio itakayosikika kwenye nyimbo yake mpya, Iyanya akiwa ni
msanii anayekubalika huko West Africa zaidi hata ya Davido, hii
inatarajiwa kumuweka Diamond Platnumz kwenye ukurasa mpya wa muziki.
Post a Comment