Na Baraka Mbolembole
Kufikia hatua ya robo fainali katika mjichuano ya kombe la dunia nchini Afrika Kusini miaka minne iliyopita, bara la ulaya lilikuwa na wawakilishi watatu tu lakini siku ya mwisho ya michuano ni Hispania na Uholanzi ambazo zilikutana katika mchezo wa fainali na Hispania kutwaa ubingwa.
Ilikuwa ni kwa mara ya kwanza kwa timu ya Ulaya kutwaa ubingwa nje ya bara lao. Hadi hatua ya nane bora inafikia Brazil, Argentina, Paraguay, Uruguay kutoka barani Amerika Kusini zilikuwa timu nne kati ya tano kutoka bara hilo kufika hatua hiyo ila ni timu moja tu iliyofuzu kwenda nusu fainali.
Brazil ilitolewa na Uholanzi baada ya kulazwa kwa magoli 2-1, Argentina ilichapwa magoli 4-0 na Ujerumani, na Paraguay walifungwa na Hispania kwa goli 1-0, Uruguay ilikuwa timu pekee kutoka Amerika Kusini , Kati na Kaskazini kufi9ka nusu fainali katika fainali hizo zilizofanyika kwa mara ya kwanza barani Afrika. Waliitoa Ghana timu pekee kati ya timu sita za Afrika iliyovuka hatua ya makundi kisha kumudu kufika hadi robo fainali kwa changamoto ya mikwaju ya penalty. Lakini kombe lilikwenda Ulaya. Vipi kuhusu Brazuca?
Michuano ya 20 ya fainali za kombe la dunia jumatatu hii zitakuwa zikiingia katika michezo ya mwisho ya hatua ya makundi ambayo itaamua timu mbili za juu kutoka katika kila kundi kutinga hatua ya 16 bora.
Baada ya michezo miwili kwa kila timu kukamilika usiku wa jumapili, tayari kuna timu ambazo zimeshakata tiketi ya kusonga mbele katika hatua ya pili, kuna timu ambazo matokeo yake ya mwisho yanaweza kuwavusha ama kuwaondoa katika michuano na tayari kuna timu ambazo zimeondoshwa katika michuano.

Waliokuwa mabingwa watetezi wa taji Hispania ilikuwa timu ya kwanza kuaga michuano baada ya kupoteza michezo yote miwili ya kwanza. Hispania iliyo katika kundi la Pili ilifungwa na Uholanzi magoli 5-1 kisha wakachapwa na Chile magoli 2-0, Cameroon iliyo katika kundi la Kwanza ilikuwa timu ya Pili kuaga michuano na ya Kwanza kwa wawakilishi watano wa Afrika baada kufungwa magoli 4-0 na Croatia katika mchezo wa Pili, awali Cameroon ambao kabla ya kwenda katika michuano wachezaji walitishia kutokwenda katika michuano kama wasingeongezewa nyongeza ya posho katika mchezo wa kwanza walichapwa goli 1-0 na Mexico.
Katika makundi mawili ya mwanzo; kundi la kwanza ambalo linajumuhisha wenyeji wa michuano, timu ya Brazil kutoka bara la Amerioka Kusini, Mexico kutoka Marekani ya Kati na Kaskazini, Croatia kutoka barani Ulaya na Cameroon. Timu tatu zina nafasi ya kufuzu kwa hatua ya mtoano. Brazil ambao watacheza na Cameroon usiku wjumatatu wanaongoza kundi wakiwa na pointi nne sawa na Mexico, tofauti ya magoli mawili kati ya Brazil na Mexico ndiyo inayowaweka juu ya kundi wenyeji wa michuano ambao watachukua pointi nyingine tatu dhidi ya moja ya timu dhaifu katika michuano inayoendelea, Cameroon ambayo haijafunga goli lolote katika michezo miwili ya mwanzo . Mexico itacheza na Croatia katika mchezo ambao mshindi atafuzu kwa hatua inayofuata.
Croatia inahitaji ushindi ili kufuzu kwa hatua ya 16 bora, wakati Mexico watahitaji satre tu ili kuendeleza rekodi yao ya kuvuka hatua ya makundi. Croatia ina pointi tatu, ni timu inayocheza mpira wa kasi na mashambulizi ya uhakika. Walifungwa MAGOLI 4-1 DHIDI YA Brazil lakini ni timu kabambe katika soka la mashambulizi. Walikataa kuingia katika mchezo wa kupooza dhidi ya Brazil na kujaribu kukimbiza mpira uwanjani jambo ambalo liliwachosha na kujikuta wakipewa kipigo chao cha kwanza kikubwa katika fainali za kombe la dunia. Wanakwenda kuikabili Mexico timu yenye kasi zaidi lakini isiyo na wafungaji mahiri.

Inaweza kuwa faida kubwa kwa Croatia ambayo inaundwa na safu kali ya mashambulizi yenye wachezaji wazoefu na viungo mahiri katikati ya uwanja, lakini ukiniambia timu gani itafuzu kutuka katika mchezo huu basi nafasi ya kwanza naipa Mexico. Wanacheza mpira wa kasi, wanashambulia bila kukata tamaaa nap engine bila uimara wa golikipa Julio Cesar wa Brazil timu hiyo ingeweza kufunga walau magoli mawili.
Ni vigumu kuwafunga. Hilo linaonesha katika takwimu zao, hadi sasa katika michuano, Mexico haijaruhusu goli lolote sambamba na Ufaransa. Hivyo inawezekana matokeo ya ushindi yakawa magumu kwao ila sare inaweza kuwa rahisi sana kwa kuwa timu hiyo ina safu imara ya muda mrefu ambayo imekuwa na uzoefu mkubwa katika fainali za koombe la dunia. Nahodha, Rafaer Marquez amekuwa katika vikosi viwili vya Mexico ambavyo viliweza kuvuka hatua ya makundi katika fainali za mwaka 2006 na zile za mwaka 2010 aliweza kuisimamia safu yote ya ulinzi kuwazima washambuliaji hatari wa Brazil wakiongozwa na kijana Neymar, Fred na Oscar. Ushirikiano na uchezaji wa uwajibikaji kwa timu za Amerika umeweza kuwasaidia hadi sasa kuwa katika nafasi ya kupeka timu nane hadi kumi katika hatua ya 16, na jambo hilo ndilo litakalo ivusha Mexico dhidi ya Croatia. Kutoka katika kundi la kwanza ni Brazil na Mexico zitakazo fuzu kwa raundi ya Pili. Wote wanatoka Amerika.
Ufaransa ilipata pointi moja katika fainali za Korea Kusini na Japan walipolazimisha suluhu dhidi ya Uruguay, wakati Italia ilipata sare mara mbili dhidi ya New Zealand na Slovakia, Nchini Afrika Kusini. Australia walikaribia kuweka mguu mmoja ndani mara baada ya kutoka nyuma na kusawazisha kisha kuongoza dhidi ya Uholanzi. ILifungwa magoli 3-2 baada ya kuzidiwa katika mbinu za kushambulia na Uholanzi, timu hiyo kutoka ukanda wa Asia ilikuwa ya tatu kuaga michuano na timu ya kwanza ya Asia. Inaweza kupeleka rekodi mbaya zaidi katika kikosi cha Hispania ambacho tayari kimesambaratishwa na Uholanzi na Chile.
Rekodi mbaya zaidi kwa safu yenye washambuliaji David Villa, Fernando Torres na Diego Costa kushindwa kufunga goli lolote. Hispania itakuwa bingwa wa kwanza kuondoka bila pointi yoypte katika fainali za kombe la dunia. Kutoka kundi la Pili, UHolanzi na Chile tayari zimekata tiketi ya kufuzu kwa hatua ya pili na zitacheza usiku wa jumatatu kuamua timu gani itakuwa nafasi ya kwanza katika kundi.
England ilifungwa na Italia katika mchezo wa ufunguzi wa kundi la tatu, mchezo ambao ulihusisha timu za Ulaya ulimalizika kwa Italia kushinda kwa magoli 2-1. England ilichapwa na Uruguay katika mchezo wa pili wa hatua hiyo ya makundi na kuondolewa katika michuano. Uzoefu umetajwa kama sababu ya kikosi cha ‘Simba Watatu’ kufanya vibaya na kuishia hatua ya makundi . Kipigo cha magoli 2-1 kutoka kwa Uruguay kilifanya nahodha wa kikosi hicho Steven Gerrard kusema kuwa walifahamu watafanya vibaya katika michuano hiyo.
Timu ambayo haikupewa nafasi kubwa ya kiufanya vizuri kutoka katika kundi hilo ndioo imekuwa ya kwanza kufuzu kiwa hatua ya 16 bora. Costa Rica ambao wanacheza fainali zao za tano za kombe la dunia kutoka Marekani ya Kati na Kaskazini ilianza michuano kwa kuifunga Uruguay kwa magoli 3-1 kabla ya kuiduwaza Italia kwa kuilaza goli 1-0 katika mchezo wa pili na kukata tiketi ya kucheza hatua ya 16 bora kwa mara ya tatu katika historia yao.
Jumanne hii timu ya Ivory Coast itakuwa ikitupa karata yake ya mwisho ili kuamua kama watafuzu kwa mara ya kwanza kwa hatua ya 16 bora ama laa!. Ivory Coast ilifuzu kwa mara ya kwanza gfainali za kombe la dunia mwaka 2006 nchini Ujerumani na ilishindwa kuvuka kundi lililokuwa na timu za Argentina, Uholanzi ( ambazo zilifuzu kwa hatua ya pili) pamoja na Serbia & Montenegro. Timu hiyo kutoka Afria Magharibi ilishinda mchezo mmoja tu na kuondolewa. ILishinda tena mchezo mmoja dhidi ya Korea Kaskazini mwaka 2010. Walifungwa na Brazil kisha walikwenda suluhu tasa na Ureno.
Katika fainali zao za tatu wachezaji wenye vipaji kama Nahodha Didier Zokora, Yaya Toure, Didier Drogba, Emmanuel Eboue, Kolo Toure na wale waliopevuka kama Salomon Kalou, Yao Gervinho Bokka na wengineo wanabeba matumaini wa timu iliyotulia na yenye uzoefu wa kutosha kufuzu kutoka kundi la tatu ambalo linajumuhisha pia timu za Colombia ( kutoka Amerika Kusini) ambayo imeshafuzu baada ya kushinda michezo yote miwili ya mwanzo, kundi hilo pia lina wawakilishi wa Asia, Japan pamoja timu ya Ugiriki kutoka barani Ulaya.
Ikiwa imeilaza Japan kwa magoli 2-1 katika mchezo wa kwanza, Ivory Coast ilikuwa nyuma kwa magoli 2-0 dhidi ya Colombia kabla ya kupata goli moja dakika za mwishoni mwa mchezo uliomalizika kwa Ivory Coast kufungwa magoli 2-1. Iacheza na Ugiriki yenye ponti moja baada ya kulazimisha suluhu dhidi ya Japan. Ugiriki ni timu nyingine ambayo haijafunga goli katika michuano inayoendelea nchini Brazil. Inaweza kufuzu kwa hatua ya pili endapo wataifunga Ivory Coast wakati, ‘ Tembo’ wanahitaji walau sare tu kufuzu kwa hatua inayofuata. Kutoka kundi hili la Tatu, Combia ( kutoka Amerika Kusini) imeshafuzu na Ivory Coast itakuwa timu ya kwanza ya Afrika kufuzu kwa hatua ya 16 bora. Hakuna timu ya Ulaya.
Kesho tutaendelea kuyatazama makundi mengine manne yaliyosalia ili kufahamu timu gani zina nafasi ya kusonga mbele na zipi ambazo tayari zimeondoshwa mashindanoni. Ni timu moja tu ya Ulaya ambayo itafuzu kwa hatua ya 16 bora kutoka katika makundi manne ya mwanzo. Je, ni timu ngapi zitafuzu kati ya timu 13 za ulaya? Brazuca imekuwa ngumu sana kwao.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.