0


Pamoja na jitihada kubwa inayofanywa na serikali katika kupambana na matukio ya ukatili kwa watoto, bado jamii inaonekana haijaipata elimu hiyo kutokana na kuendelea kuwepo kwa matukio hayo.
 
Leo mtoto mchanaga anayekadiliwa kuwa na umri wa siku moja amekutwa akiwa ametupwa eneo la Mbuyuni Kawe huku akiwa amefungwa plasta sehemu ya mdomoni na puani kumzuia kutopiga kelele pamoja na kuvuta pumzi.
 
Bw. Khamisi Hamad Bundala ambaye ni mvuvi katika eneo la Kawe, alisema tukio hilo walilijua mara baada ya mwenzao (pia mvuvi) kwenda kwenye eneo la tukio kwa ajili ya kuokota mfuko wa Rambo kwa nia ya kuwekea samaki na kisha kumkuta mtoto huyo ndani ya mfuko.
 
“Sasa baada ya kufika pale mbuyuni na kutaka kuuchukuwa mfuko wa Rambo ndio akaona kile kitoto na ndipo alipotuita na sisi na kushuhudia tukio hili. Kiukweli ni tukio baya sana na linalopaswa kupingwa na kila mmoja wetu, huu ni ukatili mbaya sana,” alisema .
“Polisi ifanye kila linalowezekana kukamatwa kwa huyo mama kiukweli huu ni zaidi ya ukatili,” alisema Edna Hamad mkazi wa Kawe.
 
Aidha, polisi  wa kituo cha Kawe walifika na kuuchukuwa mwili wa mtoto huyo.
 
Jitihada na kumpata Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni Bw. Camilius Wambura kwa ajili ya kuzungumzia tukio hilo hazikuzaa matunda baada ya simu yake ya mkononi kutopatikana.

Post a Comment

 
Top