0
Makamu Mkuu wa Chuo akijaribu kuwatuliza wanachuo hao kwa kuwaahidi kushughulikia suala lao.
Viti vikiwa vimetawanywa baada ya vurugu zilizosababishwa na mgomo huo.
WANAFUNZI wanaolipiwa na Bodi ya Mikopo katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kilichopo Mabibo Mwisho jijini Dar, leo wamegoma na kufanya vurugu wakidai kucheleweshewa fedha zao za mkopo. Mgomo huo umeanza majira ya saa 6 na nusu mchana ambapo polisi waliingilia kati kutuliza ghasia zilizokuwa zinaendelea chuoni hapo. Mpaka mtoa habari hii anaondoka eneo la tukio, bado wanachuo walikuwa wakisubiri majibu ya uongozi wa chuo hicho

Post a Comment

 
Top