0


NYOTA wa sinema za Kibongo, Irene Pancras
Uwoya amesababisha tena ! Safari hii amekinukisha
nyumbani kwa mwanaume aliyewahi kuwa mpenzi
wake ( jina tunalo) kufuatia jamaa huyo kufunga
ndoa na mwanamke mwingine na kumfanya Uwoya
kuendelea kuwa ‘ nyumba ndogo ’ .
Kwa mujibu wa chanzo chetu, ishu hiyo ilichukua
nafasi juzikati, nyumbani kwa mwanaume huyo,
Sinza- Mori jijini Dar es Salaam.
Nyota wa sinema za Kibongo, Irene Pancras Uwoya
MCHEZO ULIVYOKUWA
Chanzo kilidai kwamba , siku ya tukio , Uwoya akiwa na baadhi ya mastaa wenzake ( hawakutajwa)
kwenye kambi ya maandalizi ya kurekodi filamu mjini Bagamoyo , Pwani, alipokea simu
iliyomnyetishia kuwa , mpenzi wake huyo amefunga ndoa na mwanamke mwingine jijini Mwanza , kwa
hiyo yeye aliye tu !

UWOYA ACHANGANYIKIWA
“Uwoya alipopata salamu hizo kwa njia ya simu alichanganyikiwa ! Alianza kusema maneno ya
kumshutumu waziwazi huku akiangua kilio . Mbaya zaidi aliyemjulisha ishu hiyo alisema ndoa hiyo
ilishafungwa na si kwamba ipo kwenye maandalizi .“Akasema anaondoka kambini kumfuata jamaa yake
na kwamba atamtambua kwani nia yake ilikuwa kwenda nyumbani kwake kumfanyia fujo na huyo
mke mpya , ” kilisema chanzo hicho cha uhakika .Nyumba anayodaiwa kufanya fujo

AANZIA DUKANI
Chanzo kilizidi kudai kwamba, licha ya wasanii wenzake kumsihi asichukue hatua hiyo anaweza
kuishia polisi , Uwoya hakukubali, aliondoka kwa hasira na breki yake ya kwanza ilikuwa kwenye
duka kubwa la jamaa huyo lililopo Mikocheni , Dar ambapo alifanya fujo.
“Kule alipogundua huyo mwanaume wake hayupo ndiyo akaondoka hadi nyumbani kwake, Sinza
ambako aliendeleza fujo zake kwa kutukana na kutishia mambo mengi, ” chanzo kilisema .

HASIRA PEMBENI
Kwa mujibu wa chanzo, ni dhahiri kuwa , Uwoya aliondoka eneo hilo baada ya kuanza ‘ kujaza
nzi ’ ( watu kuwa wengi ) ambapo aliondoka mdogomdogo na kama hana hasira utadhani si yeye
aliyekuwa akichafua hali ya hewa .

MATEGEMEO YAKE
Habari za ndani ziliendelea kudai kuwa , Irene alishikwa na hasira za jamaa huyo kuoa kwa vile
alikuwa akiamini zali hilo lingetua kwake baada ya ndoa yake na msakata kabumbu wa Rwanda,
Hamad Ndikumana ‘ Katauti’ kwenda halijojo!“Uwoya alitegemea angeolewa yeye, sasa kusikia
jamaa kaoa mwanamke mwingine tena kwa siri, ilimfanya aishiwe nguvu ,” kilisema chanzo.

ALICHOAMINI
Habari zinazidi kudai kwamba, alichoamini Uwoya ni kwamba kitendo cha mwanaume huyo kuoa
kingemfanya yeye aendelee kuwa ‘ nyumba ndogo ’jambo ambalo hakupenda kulisikia hata kidogo .

UWOYA HUYU HAPA
Baada ya gazeti hili kunyetishiwa filamu nzima, lilimsaka staa huyo na kubahatika kukutana naye
maeneo ya Sinza Palestina jijini Dar ambapo alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kwamba,
alishaachana na mwanaume huyo. “Ilitokea, lakini nilishaachana naye . Unajua ishu si kwamba angenioa mimi , ila kitendo alichokifanya hakikuwa cha uungwana , ” alisema Uwoya .

AMWANGA CHOZI
Katika hali isiyotarajiwa , msanii huyo alianza kumwaga chozi bila kusema sababu hata pale
alipoulizwa kama chozi hilo lilitokana na kukumbuka tukio la jamaa yake kufunga ndoa kwa siri au la!
Uwoya: “We niache tu , nina mambo mengi sana yanayoniliza mimi .” Kwa upande wake mwanaume huyo alipopatikana kwa njia ya simu na kueleza ishu nzima alijibu kwa kifupi: “Haiwahusu .” Kisha akakata simu.

HISTORIA
Uwoya na Ndikumana walifunga ndoa Julai 11, 2009 kwenye Kanisa la Mtakatifu Joseph, Jimbo Kuu la
Dar es Salaam. Mei 8, 2011 walijaliwa kupata mtoto wa kiume aitwaye Krish . Hata hivyo , Novemba 16, 2011 kwenye gazeti hili kuliandikwa habari yenye kichwa;

NDOA YA UWOYA YAVUNJIKA.
Ndoa hiyo iliparaganyika baada ya Uwoya kudaiwa kumkataa mwanaume huyo na mpaka sasa
haijasimama tena huku mwanaume akiwa kwao , Rwanda.

Post a Comment

 
Top