Hebu
niambie...umeshawahi kujichua? Mara ngapi? Bado unaendelea na mchezo huo? Vipi,
umewahi kusikia watu wakizungumza kuhusu suala hilo? Najua unaona aibu, hasa
kama una tabia hiyo. Usiogope rafiki yangu, leo nitazungumza na wewe taratibu
halafu mwisho kabisa nitakuacha na tabasamu la nguvu!
Ndugu
zangu, wakati mwingine kuna mambo magumu kidogo ambayo baadhi ya watu
wanayaonea aibu, lakini yanaendelea kuwa tatizo kwa watu wengi. Leo
tutazungumza. Amini usiamini, asilimia 90 ya wanaofanya mchezo huo, hawapendi
hata kidogo. Kila wanapomaliza kujiridhisha huahidi kuacha, lakini baada
ya saa kadhaa kupita, wanarudi kule kule. Kama una tabia hiyo, utakuwa
unanielewa vizuri zaidi juu ya kile ninachokizungumzia hapa. Hebu twende
tukaone.
KUJICHUA
NI NINI HASA?
Kwa
Kiingereza tendo hili linaitwa ‘’ likiwa na maana ya kupiga punyeto. Hapa
nimetumia kwa ulaini kabisa; kujichua. Lugha nyepesi na rahisi kufikika kwa
wengi ni kujiridhisha! Ni kitendo cha mtu kujichezea kimahaba huku akivuta hisia
za mapenzi kwa mtu ambaye yupo mbali naye hadi anapomaliza haja zake.
Namna
ya ufanywaji inategemea zaidi na jinsi ya mazoea. Wapo wanaotumia vifaa bandia
(artificial) na wengine vifaa halisi kama aina mbalimbali za matunda ambazo
zinafanana na sehemu pacha!
Wengine
wanatumia njia wanazojua wenyewe, lakini wanaume wengi wanatumia sabuni lengo
hapa ni moja tu, unatakiwa kufahamu kwamba namaanisha kujiridhisha.
INAWEZEKANAJE
KUJIRIDHISHA?
Ni
rahisi sana kumaliza tendo la huba kwa kujifanyisha mwenyewe. Silaha kubwa
inayotumiwa na waathirika ni kuwavutia hisia watu wa jinsi pacha wakati tendo
husika likiendelea kufanyika.
Habari
mbaya kwa watu wenye mchezo huu ni kwamba, kwanza wakishaanza, inakuwa vigumu
sana kuacha. Inashindikana kwa sababu ni jambo la aibu. Si rahisi kupata
ushauri kutoka kwa watu maana ni aibu pia kumweleza rafiki yako juu ya mchezo
huo. Kutokana na hilo sasa, kinachotokea ni kwamba ‘waumini’ wa mchezo huu
wanaendelea kuwa watumwa kwa maisha yao yote. Hapa chini tutaona kwa undani
jinsi tatizo hili linavyoumiza vichwa vya wengi.
Ni
kweli hutaki kuwa mtumwa wa mchezo huu hatari? Zipo athari nyingi sana rafiki
yangu ambazo nitazieleza hapa chini.
CHANZO
NI NINI HASA?
Jambo
la kushangaza ni kwamba, hakuna mdau wa mchezo huo ambaye amefundishwa jinsi
unavyofanywa. Wengi wameanza wenyewe, tena wengine bila kujua nini
kitakachotokea, lakini baada ya matokeo kuonekana, ndiyo mwanzo wa kutopea
huko.
Kwa
vijana wa kiume, wengi huanza tabia hii wakiwa kwenye umri wa kubalehe. Mara
nyingi hutokea asubuhi wakati wa kuamka, usiku wakati wa kulala au bafuni
wakati wa kuoga.
Kwa
kawaida, mtu anapokuwa katika sehemu ya utulivu kwa maana ya kupumzika, wakati
mwingine mkono unaweza kutembea huku na huko kwenye mwili na mwisho wake bila
kutegemea mhusika anajikuta ameshaingia kwenye mchezo huo.
Huwa
kama mzaha, akiwa hajui hatma yake, lakini msisimko anaoupata ndiyo
unaomchanganya na mwisho wake anashangaa kila kitu kimemalizika. Unajua
atakachosema? Sikia: “Mh! Kumbe ndiyo mwisho wake ni hivi? Lakini kama
nimesikia starehe hivi...”
Hiyo hutokea pia wakati
wa kuoga, ambapo wakati wa kujisugua kwa dodoki, msisimko ukitokea, madhara
yanakuwa kama nilivyoeleza hapo juu.
Wenye
umri mkubwa au wa kati, huanza tabia hii hasa baada ya kuanza mchezo wa
kuangalia video za kikubwa wakiwa peke yao. Kwa sababu wanachotazama
kinahusisha msisimko wa mapenzi, basi bila kutarajia hujikuta tayari!
Hii
inafanana pia na kwa watoto wa kike, vyanzo nilivyoeleza hapo juu pia
husababisha kwa karibu sana.
Sababu
nyingine ni kunyimwa au kutotoshelezwa kimahaba na mwenzake.Wengi imewagusa,
lakini kuna makundi mawili; wapo waathirika ambao wanatamani kuachana na utumwa
huu na wengine wameathirika zaidi, kiasi kwamba hawana mpango wa kuacha.
Wengine
wameenda mbali zaidi, kwa vile hawafikirii kuachana na mchezo huu, wamefikia
hatua wanasema kwamba hakuna madhara kwa mtu anayejichua! Watu wanatetea wazi
wazi, kwamba kujichua hakuna madhara. Sikia rafiki yangu, hata anayevuta sigara
anajua kwamba ina madhara kwa afya yake, lakini ili kujifariji, atajenga hoja
kwamba, haimdhuru na badala yake inamsaidia sana kuondoa baridi na haina
kilevi.
Wakati
mvuta sigara akisema hivyo, mlevi naye atakuja na hoja kwamba, pombe inamsaidia
sana kupunguza mawazo. Kila mmoja atatetea upande wake. Ni jambo la kawaida
kabisa.
Nikiwa
naelekea kuendelea na mada yetu, rafiki yangu mpendwa kama wewe ni ‘muumini’ wa
tabia hiyo, unatakiwa kufahamu kwamba unafanya jambo HATARI sana, si tu kwa
afya yako, kisaikolojia na dhambi ya uzinifu ambayo hiyo itatokana na uhusiano
wako mwema na imani ya dini yako, NDOA yako ipo/itakuwa hatarini.
Nadhani
mnakumbuka wiki iliyopita nilieleza maana ya kujichua, namna tendo
linavyofanyika na jinsi mtu anavyoanza mchezo huo bila kutegemea. Sasa rafiki,
hebu tuendelee kwenye namna tatizo linavyokua.
UKUAJI
WA TATIZO
Mwathirika
akishazoea, hufanya tendo hilo kama sehemu ya maisha yake. Alianza bila kujua
matokeo yake, lakini sasa amejikuta akianza kuupenda na idadi ya ufanywaji wa
tendo huanza kupanda, baada ya siku tatu, siku mbili, kila siku na hatimaye kwa
siku zaidi ya mara moja.
“Kaka
Shaluwa, najichukia sana, yaani nimekuwa mtumwa kabisa wa kufanya huu ujinga.
Kwa
siku nafanya mara mbili au zaidi, lakini si chini ya hapo,” alisema rafiki
mmoja, aliyenipigia simu baada ya kusoma sehemu ya kwanza ya mada hii wiki
iliyopita.
Ukweli
ni kwamba, mfanyaji kwa vile ameshapata ‘mteremko’ wa kutimiza haja zake,
kwanza ataanza kuwadharau wanawake/wanaume, kwamba hawawezi kumtisha, kwa
sababu ana njia za kujifurahisha mwenyewe.
Pili,
hufikia hatua ya kuwachukia watu wa jinsia pacha, akiwaona kama ‘wanaringa’
hasa kama atakuwa amemshawishi kimapenzi na kukatawaliwa.
ATHARI
ZAKE
Zipo
athari nyingi sana ambazo mwathirika anaweza kuzipata kwa kuendekeza mchezo
huu. Hapa nataka nizungumze kwa herufi kubwa kabisa kwamba, ndugu zangu
usidanganyike kwamba hakuna madhara kwa kufanya mchezo huu.
Yapo
MADHARA makubwa sana ambayo yanapatikana kwa mchezo huo. Achana na propaganda
za mitaani, zenye utafiti hewa.
Sikia
nikuambie rafiki yangu, hasa wewe ambaye unafanya mchezo huo. Upo kwenye hatari
kubwa ya kushindwa kufurahia mapenzi, kwa vile mazoea ya kiungo siri chako ni
kwenye vitu ‘artificial’ zaidi ya ‘natural’.
Mwanaume
aliyezoea kujiridhisha mwenyewe, akikutana na mwanamke, hana muda mrefu sana,
kila kitu kinamalizika.
Siyo
hivyo tu, uwezo wa kurudia tendo unakuwa mdogo au unakosekana kabisa. Kinachotokea
ni kwamba, kiungo siri chake kinakuwa kimeshazoea, aina nyingine ya ‘hali ya
hewa’ hivyo kinapokutana na sehemu siri za kike, ambazo ni laini na zenye ute
mwepesi, inakuwa rahisi kumaliza ‘biashara’ mapema wakati wateja bado
wanahitaji!
Kiungo
siri cha mwanaume huwa kigumu, hivyo kusababisha maumivu kwa mwanamke kutokana
na sugu aliyoitengeneza bila kujua. Kwa kawaida viungo siri vyote ni laini sana
na vinatakiwa kubaki katika hali hiyo ili kuleta msisimko wenye usawa.
Mazoea
yoyote tofauti na yale ambayo yanatakiwa hupunguza msisiko na kusababisha mmoja
wa washiriki wa tendo la ndoa kubaki na kiu na mwenzake.
“Najuta
kuufahamu huu mchezo, kila siku ninapokutana na mume wangu, ananiacha nikiwa
sijatosheka. Kiukweli tangu amenioa, sijawahi kufurahia tendo la ndoa. Nilianza
huu mchezo zamani sana, tangu nikiwa kidato cha tano.
“Kuna
rafiki yangu mmoja nilikuwa nakaa naye bweni moja alinifundisha. Sikujua kama
madhara yake ni makubwa kiasi hiki. Ilikuwa ni shule ya wasichana tupu, kwa
hiyo akanidanganya kwamba tuachane na wanaume tujichue...kumbe alikuwa
ananisaga!” hii ni sehemu ya ushuhuda mwingine wa mchezo huo.
Athari
nyingi ambayo mtu anaweza kuipata kwa kujichua ni kumaliza ‘kazi’ mwenyewe bila
hata kwenda kazini. Akipita mtu wa jinsi pacha, ambaye ana mvuto, kazi inaishia
hapo hapo!
UPO
KUNDI GANI?
Uko
wapi rafiki yangu? Nazungumza na wewe ambaye unafanya mchezo huo, bado unataka
kuendelea nao au unatamani kuacha? Shika maneno yangu, kwamba ni HATARI
kujichua, halafu weka nia ya kutaka kuacha huu utumwa, kisha vuta subira hadi
wiki ijayo katika sehemu ya mwisho ambayo haitaacha kitu.
MFADHAIKO
Mtu
ambaye anaendekeza kazi hii, hupata mfadhaiko. Anayepata mfadhaiko, huwa
mwepesi sana wa kuwa na matamanio kwa jinsia ya upande wa pili.
Si
ajabu mtu mwenye mchezo huo, kutembelea akimwangalia mwanamke kuanzia Magomeni
hadi Manzese! Amefadhaika. Ameshazoea kumaliza kazi nzima akiwa peke yake, kwa
hiyo raha yake inabaki kuwa katika picha tu na si kitu halisi.
Macho
yanakuwa juju juu, si kwa kupenda, ni kwa sababu tayari ameshaathiriwa na
tatizo hilo. akitoka hapo, ujue moja kwa moja faragha, anaanza mambo yake.
Kelele nyingi, kumbe yupo peke yake!
Mfadhaiko
hauishii hapo, hata akiwa kwenye vyombo vya usafiri au mkusanyiko wa watu,
mwathirika huweza kumaliza ‘kazi’ kwa macho tu, tena wakati mwingine bila kuwa
na taarifa. Anakuja kugungua baadaye sana, kwamba kumbe kila kitu
kilishafanyika bila hiyari yake.
KUSHINDWA
TENDO LA KAWAIDA
Mwenye
mchezo huo, pamoja na uhodari wake wa kujifurahisha akiwa peke yake,
anapokutana na mwenzi wake faragha, kazi inakuwa si ya kiwango cha kuridhisha.
Kuna athari nyingi ambazo hujitokeza.
Kwanza,
anakosa ujasiri, hayupo tayari kuandaliwa, kumuandaa mwenzake. Kishazoea
kufanya kila kitu haraka haraka, tena kwa kutumia hisia zaidi kuliko uhalisia
wa tukio lenyewe.
Anakuwa
goigoi, anachelewa kuwa tayari, hata akiwa tayari anafika safarini mapema
zaidi. Mbaya zaidi, akifika hawezi kuanza safari nyingine. Hata kama akianza,
kuna uwezekano mkubwa wa kuishia njiani.
Baadhi
yao, hubaki wakiwa baada ya wahusika wao kuwagomea katikati ya safari. Zipo
athari nyingi zaidi ya hizo, kutegemea na namna tatizo lilivyokomaa na aina ya
jinsia.
KUFEDHEHEKA
Baada
ya hayo hapo juu kujitokeza kwenye ndoa/uhusiano wa mwathirika, kinachofuata
sasa inakuwa ni kufedheheka. Kwa bahati mbaya sana, unaweza kufanya siri mchezo
wako, lakini athari zikawa wazi kwa mwenzako.
Hata
kama hatagundua chanzo cha tatizo, lakini atagundua kwamba huna msisimko,
huwezi kazi au vyovyote vile. Wengi husema kwa hisia, humaanisha kwamba hakuna
wanachopata kutoka kwa wenzao, lakini mambo yakizidi kuwa hovyo, wanafunguka:
“Mwenzangu kila siku unaniacha na kiu, una tatizo gani?”
Kauli
hiyo rafiki yangu, inatosha kabisa kukufanya ushindwe kazi moja kwa moja.
Unajua nini? Utaanza kuwaza: “Kumbe siwezi kitu...halafu mwenzangu
ameshagundua. Nitafanyaje mimi? Mbona nahadhirika?”
Ndugu
yangu, ikifikia hapo utakuwa unamkimbia mwenzako na kwenda chemba kumaliza
biashara zako mwenyewe. Furaha ya moyo itatokea wapi? Kama ndiyo mnaishi
kinyumba au mpo ndani ya ndoa ndiyo kabisaaa!
Umeona
kazi hiyo?
UNATAKA
KUACHA?
Hakuwa
dawa kubwa sana ya kuacha mchezo huu. Najua wengi walikuwa na hamu ya kutaka
kusikia, wataachaje huu mchezo. Ndugu zangu.Usitarajie kwamba nitakuja kuingia
kwenye nafsi yako na kukuambia ACHA KUJICHUA! Ndugu zangu, nitawapa dondoo
chache sana, lakini kubwa ni kwamba ATHARI nilizotaja hapo juu zinatosha kabisa
kukubadilisha!
Hebu
nikuulize, utakuwa na hamu ya kuendelea na haya mambo kama ndoa yako itakuwa
hatarini? Nani atakubali kufedheheka? Nani atakubali kupoteza heshima yake?
Bila shaka hakuna. Pitia dondoo zifuatazo;
(i)
Badilisha utaratibu wa kulala, lala kifudifudi, badala ya chali (rejea maelezo
yangu ya awali kuhusu chanzo cha tatizo)
(ii)
Acha kuangalia mikanda ya kikubwa ukiwa peke yako.
(iii)
Kaa mbali na simulizi zinazohamasisha mapenzi, mazungumzo ya aina hiyo na
kampani za watu wanaopenda kusimulia mambo ya faragha.
(iv)
Acha mazoea ya kujishika sehemu zako za siri.
(v)
Fanya mazoezi ya viungo angalau robo saa tu kwa siku.
(vi) Juu ya yote haya,
FUTA kabisa mawazo ya jambo hilo. AMUA kwa dhati ya moyo wako, tambua na ogopa
athari ambazo unaweza kuzipata, kisha ACHA KABISA mchezo huo ili kulinda
heshima yako na kujipa furaha ya maisha
Post a Comment