Leo naomba pia niongelee kuhusu dalili ambazo zinaweza onekana kwa mwenza wako ambazo zinapelekea kujenga fikra kwamba "unasalitiwa" dalili hizo ni kama zifuatazo:-
1.Nakupenda lakini Sina Hisia nawe(Kwa wale ambao bado hawajaoana)
Hii ni dalili kwamba Mpenzi wako ana mtu mwingine nje na inawezekana
kabisa kwamba yeye ndo anapendwa zaidi yako wewe hata kama muda mwingi
upo nae! Anakutumia tu huyo!
2.Sisi ni Marafiki tu!
Kwa amnbao bado hawajaoana Ukimuuliza Mpenzio unanichukuliaje au mimi ni
nani kwako anakuwa anasuasua sana sana utaambiwa ni marafiki tu.Na kwa
ambao tupo katika Ndoa ukiuuliza vipi mbona nakuona una mazoea ya karibu
mno na mtu fulani? Utaambiwa ni Rafiki tu!
3 Nahitaji muda wa kufikiria kuhusu hisia zangu!
Hili nijibu tosha kwamba Kuna Mwenzio ambaye anamchanganya akili mpenzi
wako na ndio maana anakuwa hivyo! Anza kukaa tayari au mguu nje, mguu
ndani!
4.Mabadiliko ya Ratiba za Kazi
Kwa wale ambao tupo ndani ya ndoa au mahusiano ya muda mrefu, utaliona
hili, mara kurudi late sana, ubize umekuwa mwingi mno hadi weekend! Na
dharula za kikazi zisizoisha!
5. Kutumia Muda Mwingi katika Computer
Kama ameweza kujizuia kutoka toka hovyo, basi anaweza kuwa mtumiaji
mzuri na wa muda mrefu wa Computer, atakaa hapo ata chat na kuongea na
wezi wako tani yake, na unaweza usilijue hili kwani atakuambia ana kazi
za ofisini anamalizia!
6. Simu za Siri, Simu kuwa locked!
Siku hizi simu zimekuwa nyingi, za usiku, mara simu ikipigwa ananyanyuka
kwenda chumbani au kujificha kidogo, mara simu ikipigwa inakwatwa! Na
ya kufanana na hayo!
7. Tabia yoyote yenye kutia Mashaka!
Waswazi wanasema "Wasiwasi ndo Akili" Basi wasiwasi wako huenda ukakupa
akili juu ya nini kinachoendelea na ukapata njia ya kuubaini ukweli!
Ukiyaona haya au ya kufanana na haya kaa ukijua kuna kidudumtu
kinawala na kitawatenganisha, Ni vyema ukachukua hatua! Pia Jiandae
Kudanganywa!
Post a Comment