Home
»
MAPENZI
» FAHAMU MAMBO YANAYOWEZA KUSABABISHA UPENDO UKAPUNGUA KWA MPENZI WAKO:

Yafuatayo ni baadhi ya mambo/ vitu vinavyopunguza mapenzi katika mahusiano ya kimapenzi1. UGOMVI WA KILA SIKUKwenye ulimwengu wa Mapenzi hakuna kitu
kibaya kama kutoweka kwa amani kaa ukijua mapenzi ni matamu na yanaraha
iliyoambatana na furaha hakuna mtu anaependa kuishi bila ya kuwa na
furaha hivyo ikitokea katika mahusiano wapenzi hawapatani na kila mmoja
wao hataki kukubali kosa wote wanajiona wapo sahihi halafu mwisho wa
siku wanapatana ghafla bila kuombana msamaha ni wazi kabisa kosa bado
litakuwa halijarekebishwa hivyo ni rahisi kutokea tena ugomvi na
ikitokea kila siku penzi lenu linatawaliwa na ugomvi nirahisi penzi
kukosa muelekeo na kila mmoja wenu akahisi hapati amani ya pumziko la
moyo kwa mpenzi wake hivyo mnaweza kujikuta upendo unapungua katika
penzi lenu na matokeo yake moyo wako utakuwa bado haujapata kimvuli cha
burudani za mahaba utajiwa na fikra za kutaka kumtafuta mpenzi mwingine.
2. KUTOKUBALI HALI HALISI YA MPENZI WAKO:Hii ni moja kati ya sababu kubwa
inayopunguza mapenzi kwa kiasi kikubwa, walio wengi katika mahusiano
siku zote hutegemea faida tu kwa upande wake pasipo kumjali mwenzake
zaidi hili hutawala katika upande wa kifedha, unaweza kumkuta mtu
anampenda mpenzi wake pindi awapo na hela na kama ikitokea siku mpenzi
wake kakosa hela basi inaweza kutokea hali ambayo si yakawaida. Kikubwa
naomba utambue kuwa mapenzi sio pesa ila pesa ni sehemu moja wapo ya
mapenzi ambayo hutumika katika njia ya kuboresha mapenzi nachoweza
kukwambia jaribu kuwa muelewa, kubaliana na hali halisi ikitokea
unashida ya pesa au kitu chochote toka kwa mpenzi wako muombe kama
anacho atakupa au kukununulia na kama hana atakuambia kwamfano: "Mpenzi
kwa sasa hali yangu iko chini kidogo naomba univumilie kati ya hizi siku
2 nitakupa" utakapo ambiwa hivi kuwa nasubira mvumilie ila kama
hutojali hali ile na ukaenda kinyume na maombi yake niwazi kabisa hisia
zake zitamtuma wewe si mkweli kwake na nirahisi kupunguza upendo kwako
3. KWENDA KINYUME NA HISIA / MATAKWA YA MPENZI WAKO:Mpendwa napenda ufahamu katika mapenzi
kila mmoja huwa na tabia yake na sheria zake katika mapenzi hivyo ni
vizuri mkiwa kama wapenzi katika mahusiano yenu muweze kusomana tabia na
kila mmoja wenu aweze kutambua mpenzi wake anapenda nini na nini
hapendi tukija katika upande wa sheria pia ni vizuri kama kila mmoja
wenu aweze kumueleza mwinzie vitu anavyotaka vifuatwe katika mahusiano.
Mapenzi yanaweza kupungua katika hili iwapo kama itatokea kuna mmoja
wapo kati yenu anahitaji afanyiwe vitu fulani lakini vinakuwa
havitekelezwi kwa mfano: Mpenzi wako anaweza akakuomba kushiriki tendo
la ndoa akiwa na hamu anakwambia "Dear leo naham nawewe mpenzi nahitaji
kulifurahia penzi lako usiku wa leo" unamjibu "Umeisha anza nawewe mimi
sijisikii bwana!". Kinapotokea kitu kama hiki ni dhahiri kwamba
umeshindwa kumtimizia mpenzi wako mahitaji yake ndipo upendo wake kwako
utaanza kupungua hatima yake ataamua kutafuta mtu mwingine kwani atahisi
kama kwako hapati anavyovitaka.
- mpenzi msomaji wa ukurasa huu hivyo ndivyo vyanzo
vikuu vinavyoweza kupelekea penzi likapungua kwa kiasi kikubwa ingawa
zipo sababu nyingi zinazoweza kumfanya mtu akapunguza mapenzi kwa mwenzi
wake ila hizo nilizozieleza ni kuu zaidi kitu kikubwa ninachoweza
kukushauri kuwa makini katika mapenzi jitahidi kumridhisha mpenzi wako
mtambue tabia yake na umfanyie yatakayompendeza.
Post a Comment