Watu wakiwa wanazama katika mapenzi , mapenzi yanakua ni sababu kuu ya mahusiano kwa kipindi hicho na wanasahau tofauti zao zinazoweza kuwafanya wakaachana.Ingawa pale tofauti hizo zinapojitokeza kutengana kwa mahusiano hayo kunaanza kupiga hodi. Hizi ndio sababu kuu zinazosababisha mahusiano na ndoa nyingi kuvunjika.
Kutobaki njia kuu (ku-cheat na uzinzi)Uzinzi ndio chanzo kikuu cha kuvunjika kwa ndoa na mahusiano ambapo ku-cheat pia kunaua karibu kila mahusiano pale inapofikia hatua ya kujionesha.
Unyanyasaji wa kimwili na kiakili
Siku za karibuni idea ya mwanamke kua sawa na mwanaume imezidi kukua na kufanya mahusiano mengi kua katika njia panda na mwisho wa siku kuvunjika.ikiwa ni sababu ya kawaida, manyanyaso haya huletwa na tabia za kujiona mnyonge kwa mtu mmoja au wote katika mahusiano kitu kinachochangia kukandamizwa,kushikiliwa na kutishiwa. watu wote wanashidwa kuvumilia mambo haya na kuamua kuvunja mahusiano.
Ubinafsi
Baada ya hatua za mwanzo za mahusiano kuisha, watu wengi huanza kukuza hisia za ubinafsi ambayo baadae huanza kubomoa uhalisia wa mapenzi na kusababisha uhusiano kuvunjika.
Kugombana na kubishana kusikoisha
Kama watu walio kwenye mahusiano watashidwa kukubali kuelewana husababisha mabishano na kugombana ambayo pia hufanya hali isiwe shwari kwenye mahusiano.Hii husababisha mahusiano kukosa mwelekeo na mwisho wa siku kuvunjika.
Wivu
Kuvunjika kwa ndoa mara yingine inachangiwa na wivu na kusababisha hali mbaya sana. ukianza kufikiria mwenza wako anaweka umakini mwingi kwa mtu mwingine utaanza kumuona havutii tena na mwisho wa siku kuvunja uhusiano.
ili kufanya uhusiano wako ukue na uwe imara ni muhimu kukwepa vitu hivi na utaishi kufuatana na ndoto zako.

Post a Comment